Wajumbe wa bodi ya Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLa), wakifuatilia mazungunzo kwa njia ya mtandao na watu wa Kenya, leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa TaGLA, Bwana Charles Senkondo akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue katika kituo cha taarifa za maendeleo (TDIC), alipotembelea ofisi hizo, leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wa tatu kushoto), akiangalia namna majadiliano yanavyofanyika kwa mfumo wa kutumia mtandao katika Ofisi za Wakala wa Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLa), wakati wa ziara yake leo, jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Menaja wa Tecknolojia TaGLA, Bwana Emmanuel Tessua na wa pili ni Mkurugenzi Mtendaji wa TaGLA, Bwana Charles Senkondo.
Na Lorietha Laurence- MAELEZO
19.12.2014
SERIKALI imejidhatiti
katika kuboresha huduma za mawasilano kwa
Njia ya Mtandao (TEHAMA) ili kurahisisha
utendaji wa shughuli mbalimbali za kiserikali.
Akiongea na wajumbe wa
bodi ya Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), jijini Dar es Salaam,
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue
amesema lengo la Serikali ni kuongeza ufanisi kwa watumishi na jamii kwa
ujumla kujifunza na kuwasilisha mada
mbalimbali kupitia mtandao.
Balozi Sefua amesema
kuwa serikali na taasisi zake mbalimbali hazina budi kutumia wakala wa Mafunzo
kwa Njia ya Mtandao kufanya shughuli zake zote zinazotekelezeka kwa njia ya
Videoconference na Mafunzo ya Masafa ili kupunguza gharama.
“Lengo kuu la Serikali
ni kurahisisha mawasilino baina ya watumishi na jamii ili kupunguza usumbufu wa
safari ndefu kutoka sehemu moja kwenda nyingine na pia kuokoa muda, na urahisi
wa upatikanaji wa huduma kwa wananchi” alisema.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mtendaji wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), Bwana Charles
Sekondo, amesema ofisi yake imekuwa
ikitekeleza majukumu kwa ufanisi kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali wanaojihusisha na mafunzo kwa njia ya mtandao
ili kwenda sambamba na maendeleo ya teknolojia duniani katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kijamii
na kiserikali.
“Wakala wa Mafunzo kwa
Njia ya Mtandao imerahisisha sana
mawasiliano baina ya serikali, wizara, idara , wakala wa Serikali, pamoja na
Sekta binafsi katika kuboresha uweledi
kiutendaji kupitia utawala bora, anuai
za jamii, maswala ya afya na mazingira” alisema Sekondo.
Katika Ziara hiyo
Katibu Mkuu Kiongozi alitembelea maeneo mbalimbali ya ofisi ya Wakala wa
Mafunzo kwa njia ya Mtandao ikiwemo
Sehumu ya Huduma za Video Conference,
Chumba cha Maabara za Kompyuta na kituo cha taarifa za maendeleo (TDCI).
Mtandao wa TaGLA,unajukumu
la kuwajengea uwezo watumishi wa wizara, idara na wakala wa serikali pamoja na
sekta binafsi katika nyanja mbalimbali ikiwemo , mafunzo ya midahalo kwa njia ya video ya hapa
nchini na nchi nyingine, midahalo kwa
njia ya mtandao, mafunzo ya ana kwa ana na mafunzo kwa njia ya uongozi.
No comments:
Post a Comment