*Kutambulisha filamu zao katika muonekano mpya
Mratibu wa Kampuni ya wasanii wa Bongo Movi ya usambazaji filamu ya Steps Entertainment, Myovela Mfwisa, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu kampuni hiyo, kutambulisha filamu zao katika muonekano mpya. Kutoka kushoto ni wasanii Jacob Stephen 'JB', Ofisa uhusiano wa kampuni hiyo, Selles Mapunda na Mzee Majuto. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)Mratibu wa Kampuni ya wasanii wa Bongo Movi ya usambazaji filamu ya Steps Entertainment, Myovela Mfwisa, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu kampuni hiyo, kutambulisha filamu zao katika muonekano mpya. Kutoka kushoto ni Mzee Majuto, Mohamed Zubery 'Niva' (wa tatu) na Produza Simon Mwapagata.
Wasanii wa Bongo Movi, wakionesha muonekano tofauti wa filamu zao ambazo zitaboreshwa na Kampuni yao ya Steps Entertainment ili zionekane katika muonekano mpya kwa ajili ya kuboresha mauzo na maslahi yao, pia kupunguza wizi wa kuzirudufu unaofanywa na vijana mitaani hali inayowasababishia kupata kipato kidogo.
Wasanii wa Bongo Movi, wakionesha muonekano tofauti wa filamu zao ambazo zitaboreshwa na Kampuni yao ya Steps Entertainment ili zionekane katika muonekano mpya kwa ajili ya kuboresha mauzo na maslahi yao, pia kupunguza wizi wa kuzirudufu unaofanywa na vijana mitaani hali inayowasababishia kupata kipato kidogo.
Mratibu wa Kampuni ya wasanii wa Bongo Movi ya usambazaji filamu ya Steps Entertainment, Myovela Mfwisa, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, alipokuwa akielezea kuhusu kampuni hiyo, kutambulisha filamu zao katika muonekano mpya. Kutoka kushoto ni wasanii Jacob Stephen 'JB', Ofisa uhusiano wa kampuni hiyo, Selles Mapunda na Mzee Majuto.
Msanii wa Bongo Movi, Jacob Stephen 'JB', akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati wasanii hao walipokuwa wakielezea kuhusu Kampuni yao ya usambazaji filamu ya Steps Entertainment, kutambulisha filamu zao katika muonekano mpya. Kulia ni Mratibu wa kampuni hiyo, Myovela Mfwisa.
Msanii na Mwandaaji wa flamu, Rammy Galis akielezea jambo wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari, Kampuni ya wasanii wa Bongo Movi ya usambazaji filamu ya Steps Entertainment, kutambulisha filamu zao katika muonekano mpya.
Msanii na Mwandaaji wa flamu, Rammy Galis akielezea jambo wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari, Kampuni ya wasanii wa Bongo Movi ya usambazaji filamu ya Steps Entertainment, kutambulisha filamu zao katika muonekano mpya. Kulia ni msanii Jacob Stephen 'JB'.
KAMPUNI ya usambazaji wa filamu bora Tanzania ya Steps Entertainment Ltd inatarajia kutoa bidhaa mpya za filamu kwa mwaka ujao wa 2015 filamu zenye ubora muonekano mzuri huku pia kuwaletea walaji bei rafiki kutoka kampuni bora ya usambazaji wa filamu Tanzania Steps Entertainment Ltd.
Steps Entertaiment Ltd ni Kampuni ilioanzishwa mwaka 2007 nchini Tanzania, makao yake makuu yako jijini Dar Es salaam, Kampuni hii inajishughulisha na usambazaji wa filamu za Kitanzania maarufu kwa jina la BONGO MOVIES
Tangu kuanzishwa kwake Kampuni ya Steps Entertainment Ltd imekuwa mdau mkubwa katika kukuza tasnia ya filamu nchini Tanzania, mpaka sasa ndiyo kampuni kubwa ya usambazaji wa filamu hapa nchini
Kampuni ya Steps Entertainment kupitia imefanikiwa kutoa ajira nyingi kwa wadau mbalimbali wa tasnia ya filamu, wakiwemo waandaaji wafilamu Waigizaji, Wasambazaji wakubwa kwa wadogo, Wauzaji wa rejareja n.k. Pia Steps Entertainment ltd imefanikiwa kuvuka mipaka na kuzifikisha sinema za Kitanzania katika mataifa mbalimbali ya nje na katika luninga za kimataifa.
Kwa mafanikio hayo ya usambazaji Kampuni ya Steps Entertainment imechangia sana katika kuitangaza Utamaduni na lugha ya Kiswahili, Kuongeza ajira kwa wasanii na kuchangia pato la taifa kupitia ulipaji wa kodi itokanayo na mauzo ya filamu.
Hivi karibuni kumetokea kukithiri kwa filamu za kigeni ambazo zimekuwa zikiuzwa kwa bei ya chini kuliko filamu za ndani yaani filamu zetu za Kitanzania. Sambamba na hilo pia kumetokea ongezeko kubwa la makundi ama watu wanao fanya uharamia wa filamu za Kitanznia na Kuziuza kwa bei ya chini mno, ambapo wananchi wamekuwa wakizinunua kwa wingi kutokana na kuwa ni za bei rahisi sana. Mambo haya na mengine mengi yamechangia sana kuwakosesha wadau halali kipato kitokanachotokana na jasho la kazi zao na badala yake kuwanufaisha wachahe wanaofanya uharamia wa kazi hizi za filamu za Kitanzania.
Baadhi ya wadau wa filamu za Steps waliishauri Steps Entrtainment ltd kujaribu kupunguza bei za filamu zake ili kuona kama inaweza kusaidia kupunguza uharamia wa filamu hizi na kuongeza mauzo ya nakala halisi za Kampuni ya Steps Entertainment ltd.
Kampuni ya Steps Entertainment ltd ilifanya utafiti ili kujua ni jinsi gani filamu zinatoka mbali nje ya nchi na bado zinawafikia walaji kwa bei ya chini sana pia kampuni ilifanya utafiti kujua kwa nini wateja wengi ambao hapo awali walikuwa wananunua nakala halisi za filamu za kitanzania sasa weni wananunua filamu za nje ama wananua filamu za kitanzania kutoka kwa maharamia (yaani wengi wanafanya biashara ya kuuza filamu fake)
ni baada ya utafiti huo ndipo Kampuni ya Steps Entertainment iliamua kujibana na kufanikiwa kuingiza na kufunga mtambo mkubwa wakisasa wa kutengeneza cd/dvd na kuzirekodi hapa hapa nchini tofauti na siku za nyuma ambapo ilikuwa inaagiza cd/dvd kutoka nje ya nchi na kuja kuzirekodi tu, sambamba na mtambo huo pia kampuni hii imeamua kubuni kifungashio kipya yaani kasha za cd/dvd, kasha ambazo ni za bei nafuu, zinamuonekano mzuri zaidi, ni rahisi kuhifadhi, ni rahisi kusafiriha na ni rafiki wa mazingira.
Mtambo mkubwa na wa kisasa pamoja na kifungashio kipya vimepunguza gharama za kuzalishia nakala za dvd na cd na hivyo Steps Entertainment td imeona ni vyema sasa kutekeleza ushauri wa wadau wake wa kupunguza bei za filamu zake.
Kampuni ya Steps Entertainment inaamini kuwa kitendo cha kupunguza bei za filamu zake
1. Kinaonyesha moyo wa uzalendo lakini pia kitapandisha mauzo ya filamu za Kitaznzania ambapo kwa ujumla wake itaongeza kipato kwa wasanii na kuchangia pato la taifa.
2. Kitapunguza uharamia wa filamu kwa kuwa bei itakuwa chini hivyo wateja watakuwa na uwezo wa kununua nakala halisi.
3. Kitaziwezesha library zinazokodisha filamu kuacha kukodisha na badala yake kuanza kuuza mojakwa moja.
Hivyo basi Kampuni ya Steps Entertainment inamaliza mwaka 2014 na kuingia mwaka 2015 kwa kubororesha bidhaa zake, zikiwa katika ubora na muonekano wa kuvutia kwenye kasha la bahasha ngumu, bidhaa hizi zitamfikia mlaji kwa bei ya 1,500/= tu, bei hii ni kwa filmu zitakazo kuwa katika kifungashio kipya pekee, filamu zitakazo kuwa katika kifungashio cha zamani yaani kasha la plastiki zitaendelea kuuzwa kwa bei ileile na wateja watakuwa huru kuchagua aina ya kifungashio pale wanaponunua nakala za filamu za steps
Hivyo basi Steps Entertaiment imeanzisha kampeni maalum ya “Faidika na Steps kwa bidhaa bora, Wasanii nyota, na Filamu Bora, KWA BEI POA”.
Kampuni ya Steps Entertainment inawaomba wadau wote kuendelea kuzienzi filamu za kitanzania ili kukuza kipato cha wasanii na taifa kwa ujumla , kutangaza lugha ya Kiswahili na utamaduni wa kitazania.
Kampuni ya Steps Entertainment itaandika bei kwenye makasha na hivyo inaiomba jamii isikubali kuuziwa filamu za steps tofauti na bei iliyoandikwa kwenye kasha. Na pia Steps inawakaribisha wasmbazaji wengine wazalishe dvd na cd zao katika kiwanda cha steps mbapo watalishiwa kwa bei nafuu saana ili nawao pia waweze kupunguza bei za filamu zao kama wataona inafaa kufanya hivyo ili kusaidia katika kupunguza uharamia wa filamu za Kitanzania
Kampuni ya Steps Entertainment ltd na wadau wake kwa pamoja tunaiomba Serikali Chini ya Rais wetu Mpendwa Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete itusaidie kupambana na uharamia wa filamu ambao kwa sasa umevuka mipaka, Kila leo waandaaji wa filamu na wasanii wanaendelea kuwa masikini, wakati kazi zao zimezagaa nchi nzima na wala maharamia hawaoni kuwa ni kosa kufanya hivyo.
Ndugu Wanahabari Steps Entertainment ltd pamoja na wadau wake wanaomba sana muifikishie jamii taarifa hii.
Ahsanteni
MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI AFRIKA
Dilesh Solanki
Mkurugenzi Mtendaji Steps Entertainment Ltd.
No comments:
Post a Comment