TANGAZO


Friday, December 5, 2014

Wahitimu 130 wa Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU), watunukiwa Tuzo kwa kufanya vizuri kwenye masomo yao

Onesmo Charles ambaye ni mmoja wa wanafunzi 130 waliofanya vizuri katika masomo katika Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU), akijaribu kifaa cha kisasa cha kupimia ardhi, viwanja na ramani za nyumba alichozawadiwa Kampuni ya Hightech Systems (T) Limited katika hafla ya kuwakabidhi zawadi na tuzo wanafunzi hao bora  iliyofanyika katika chuo hicho leo ikiwa ni sehemu ya mahafali ya nane ya chuo hicho yatakayofikia kilele kesho kutwa Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi Dar es Salaam (ARU), Idrissa Mshoro (kulia) akimkabidhi mwanafunzi Onesmo Charles kifaa cha kisasa cha kupimia ardhi, viwanja na ramani za nyumba chenye thamani ya sh. mil. 35  baada ya kuwa mmoja wa wanafunzi 130 waliofanya vizuri katika masomo. Hafla ya kuwakabidhi zawadi wanafunzi hao bora  iliyofanyika katika chuo hicho leo, ni sehemu ya mahafali ya nane ya chuo hicho yatakayofikia kilele kesho kutwa kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi Godfrey Ntaki wa Kampuni ya Hightech Systems (T) Limited.  iliyotoa zawadi hiyo. (PICHA ZOTE NA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
Onesmo akipongezwa na wanafunzi wenzake.
Onesmo akiwa katika picha ya pamoja na wenzake
Cheti alichotunukiwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Ipyana Mwangoka akikabidhiwa zawadi ya cheti.
Jonathan Kansheba akitunukiwa cheti.
Joyce Kasenga akipatiwa tuzo ya cheti.
Mariam Maringe akipatiwa tuzo.
Rashid Ngenyi akipatiwa tuzo ya cheti.
Rebecca Milano alipatiwa tuzo tano.
Tadeus Rudaichi akipokea tuzo.
Asha Muhali alituzwa tuzo tano.
Anthony Mwashilingi akizawadiwa.
Bibian Abel akizawadiwa.
Faraja Ally akizawadiwa cheti.
Ikupa Mwakisole akipokea tuzo ya cheti.


Sehemu ya wanafunzi waliotunukiwa tuzo.
 Meza kuu wakiwa katika mahafali hayo.
Wanafunzi wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa chuo hicho pamoja na wafadhili.
Picha ya Pamoja
Picha ya Pamoja.

No comments:

Post a Comment