*Ni kwa njia ya kielektroniki kupitia huduma ya M-Pesa
* Imelenga wanaohitaji huduma katika sekta ya usafiri wa anga
na hoteli
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma
wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia (katikati), akiongea na waandishi wa
habari(hawapo pichani)wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Vinjari na M PESA itakayowawezesha
wateja wa mtandao huo kufanya malipo ya huduma katika sekta ya usafiri wa
anga,mahoteli na utalii kwa njia ya kieletroniki huduma hiyo inapatikana
kupitia tovuti ya vinjari. Wengine katika picha maafisa waandamizi wa tovuti ya
vinjari kushoto ni Manase Banduka
Mkurugenzi wa Uendeshaji,kulia Mkurugenzi Mtendaji Andrew Mboma.
Mkurugenzi Mtendaji wa tovuti ya Vinjari Andrew Mboma (kulia), akifafanua
jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani), wakati wa uzinduzi
wa huduma mpya ya Vinjari na M PESA itakayowawezesha wateja wa Vodacom
Tanzania kufanya malipo ya huduma katika sekta ya usafiri wa anga,mahoteli na
utalii kwa njia ya kieletroniki huduma hiyo inapatikana kupitia tovuti ya
vinjari, Wengine katika picha Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa
Umma wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia(katikati) kushoto ni Manase Banduka Mkurugenzi wa Uendeshaji.
.Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Rosalynn
Mworia(kushoto)akipongezana na maafisa waandamizi wa tovuti ya vinjari (katikati
) Manase Banduka Mkurugenzi wa Uendeshaji (kulia ), Mkurugenzi Mtendaji wa tovuti
hiyo Andrew Mboma wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Vinjari
na M PESA itakayowawezesha wateja wa Vodacom
kufanya malipo ya huduma katika sekta ya usafiri wa anga,mahoteli na utalii kwa
njia ya kieletroniki huduma hiyo inapatikana kupitia tovuti hiyo.
Na Mwandishi wetu
KATIKA
kuzidi kurahisisha huduma za malipo wakati
tukielekea msimu wa sikukuu za Krismas na Mwaka Mpya,kampuni ya mawasiliano ya
Vodacom Tanzania leo imezindua huduma mpya ya kufanya malipo kwa njia ya kielektroniki.
Huduma hii
mpya inayozinduliwa leo inajulikana kama Vinjari na M-Pesa ambayo
itawawezesha wateja wa Vodacom kufanya malipo ya huduma katika sekta ya usafiri
wa ndege na utalii kwa njia ya kieletroniki kama ambavyo yamekuwa yakifanyika
kwa kutumia kadi mbalimbali za kufanyia malipo kimataifa.
Akiongea
wakati wa uzinduzi wa huduma hii Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa
Umma wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia amesema huduma hii kwa kuanzia
itafanyika kwa kushirikiana na mtandao wa malipo ya kieletronikali nchini
ujulikanao kama Vinjari.co.tz ambao unafanya kazi na zaidi ya taasisi 300 za
kutoa huduma yakiwemo mahoteli ya utalii
na makampuni mbalimbali yanayotoa huduma hususani za masuala ya utalii na sehemu za mapumziko na
burudani.
“Kadri
siku zinavyozidi kusonga mbele tunazidi kushuhudia mapinduzi makubwa ya
kiteknolojia hususani katika masuala ya biashara, Vodacom tumeona umuhimu wa
kuanzisha huduma hii ili kuwawezesha wateja wetu kufanya miamala yao kwa njia
ya kieletroniki kupitia huduma ya M-Pesa ili kwenda na wakati zaidi. Kwa
kuanzia tutatoa huduma hii kupitia mtandao
mpana wa malipo ya kielektronoki
wa vinjari.co.tz na kadri siku zitakavyosonga mbele tutazidi kuboresha huduma
hii,” alisema.
Aliongeza
kuwa Vodacom inaelewa kuwa idadi kubwa ya Watanzania hawana kadi za kimataifa
za kufanya miamala ya malipo kwa njia ya kielekroniki ndio maana imekuja na
huduma hii ikiwa inawalenga wateja wetu wanaotumia huduma ya M-Pesa.
Naye Mkurugenzi wa Vinjari.com,Andrew Mboma
amesema ili kupata huduma hii mteja anaingia katika sehemu ya kawaida ya
kufanya miamala ya M-Pesa kwenye simu yake atakuta sehemu inayomuelekeza jinsi
ya kupata huduma kupitia Vinjari na M-Pesa ambapo ataweza kufanya muamala kwa
kadri ya huduma atakayokuwa anahitaji na
atakatwa fedha kutoka akaunti yake ya M-Pesa kulipia huduma hiyo na malipo
kidogo ya kutumia huduma hiyo. Maelezo zaidi yanapatikana kwa kutembelea tovuti
ya vinjari.co.tz
Katika
miaka ya karibuni kumekuwepo na ongezeko kubwa la matumizi ya simu za mkononi
nchini ambapo pia kumekuwemo na ongezeko la watumiaji wa mtandao wa internet.
Inakadiriwa
kuwa zaidi ya watanzania milioni 28 wanatumia huduma za simu za mkononi ambapo
zaidi ya watanzania milioni 6 wanatumia huduma za internet.
No comments:
Post a Comment