TANGAZO


Saturday, December 6, 2014

Uingereza kuweka jeshi lake Bahrain

Jeshi la Uingereza likiwa katika gwaride.Uingereza imeafikiana na Bahrain kuweka kituo chake cha jeshi nchini humo.
Uingereza imesaini makubaliano na Bahrain ya kujenga kituo cha jeshi la wanamaji nchini humo ambacho kitakuwa ndicho kituo cha kwanza cha jeshi la Uingereza eneo la mashariki ya kati tangu iondoke eneo hilo mwaka 1971.
Makubaliano hayo yaliafikiwa baada ya mieizi kadhaa ya mazungumzo.
Waziri wa ulinzi nchini Uingereza Michael Fallon alisema kuwa kituo hicho kitaliwezesa jeshi la wanamaji la Uingereza kuleta udhabiti eneo la Ghuba.
Mwandishi wa masuala ya usalama wa BBC anasema kuwa makubaliano hayo yanafanyika wakati nchi za Ghuba zinakabiliwa na tishio kutoka kwa wanamgambo wa Islamic State.

No comments:

Post a Comment