TANGAZO


Friday, December 12, 2014

TBL yatoa sh. milioni 18 kusaidia ukarabati wa miundombinu iliyoharibika Soko la Machinga Ilala, Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (kulia) akikabidhi hundi yenye thamani ya sh. mil. 18.9, kwa  Mkurugenzi wa Kampuni ya Gotam General Traders, Winner Taluka (wa pili kushoto) kwa ajili ya kusaidia ukarabati wa miundombinu ya maji iliyoharibika baada ya Soko la Mchikichini Ilala  kuteketea kwa moto. Wanaoshuhudia hafla hiyo iliyofanyika Dar es Salaam jana, kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa soko hilo, Rehema Matali,  Mjumbe wa Kamati ya Maji  katika soko hilo, Christopher Mbowe pamoja na Kaimu Mweka Hazina wa Manispaa ya Ilala, Ulinyelusya Mwamtobe.
Kilindo akikagua kisima cha maji ambacho miundombinu yake iliharibika baada soko hilo kuteketea kwa moto. Kisima hicho cha maji awali kilijengwa kwa msaada wa TBL.
Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (kushoto),  akiangalia chemba ambamo kuna pampu ya maji iliyoharibika wakati wa janga la moto lililoteketeza Soko la Mchikichini Ilala, Dar es Salaam, ambapo jana kampuni hiyo ilikabidhi msaada wa sh. mil. 18.9 za kukarabati miundombinu ya maji katika soko hilo lenye wafanyabiashara wanaokadiriwa 7000.
Kaimu Mweka hazina wa Manispaa ya Ilala, Mwamtope akitoa shukurani kwa TBL kwa msaada huo wa kukarabati miundombinu.
Kilindo 9wa pili kulia) akijadiliana jambo na  Rehema Matali kuhusu kalo linalotumiwa na Mama Lishe, Baba Lishe  kuoshea vyombo.
Moja ya mabomba yaliyoharibika na kutakiwa kufanyiwa matengenezo.
Kilindo akitoka kukagua miundombinu ya maji katika soko hilo.

No comments:

Post a Comment