TANGAZO


Tuesday, December 2, 2014

Rais Kikwete amwapisha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali leo Ikulu


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Musa Juma Assad Ikulu jijini Dar es Salaam leo Disemba 2, 2014.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu mpya wa Hesabu za Serikali Prof. Musa Juma Assad akisaini hati ya kiapo chake mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete mara baada ya kuapishwa leo Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Aron Msigwa –MAELEZO)         


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitia sahihi yake kwenye nyaraka baada ya kumuapisha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Musa Juma Assad Ikulu jijini Dar es Salaam leo.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi vitendea kazi baada ya kumuapisha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Musa Juma Assad Ikulu jijini Dar es Salaam leo Novemba.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Musa Juma Assad baada ya kumuapisha  Ikulu jijini Dar es Salaam leo.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali, Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda, Jaji Mkuu Mhe Mohamed Chande Othman, Spika Anne makinda na Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Musa Juma Assad Ikulu jijini Dar es Salaam leo.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na familia ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Musa Juma Assad Ikulu jijini Dar es Salaam leo.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Musa Juma Assad na CAG Mstaafu Bw. Ludovick Utouh Ikulu jijini Dar es Salaam leo.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Musa Juma Assad na wafanyakazi wa ofisi ya CAG  Ikulu jijini Dar es Salaam leo Disemba 2, 2014. (Picha zote na Ikulu)  
Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashilila akisalimiana na Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman wakati wa hafla fupi ya kuapishwa kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu mpya wa Hesabu za Serikali iliyofanyika leo Ikulu jijini Dar es salaam, Kulia ni Spika wa Bunge Mh. Anne Makinda. (Picha zote chini na Aron Msigwa –MAELEZO)         
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mh. Zitto Kabwe akisalimiana na Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya wakati wa hafla fupi ya kuapishwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu mpya wa Hesabu za Serikali Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu mpya wa Hesabu za Serikali Prof. Musa Juma Assad(wa pili kutoka kushoto) na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Anne Makinda akizungumza jambo na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali mara baada ya kuapishwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu mpya wa Hesabu za Serikali Ikulu jijini Dar es salaam.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Anne Makinda akizungumza na waandishi wa habari kuhusu  ushirikiano uliopo kati ya Ofisi yake kupitia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali katika kujenga Mfumo wa kisasa wa ukaguzi wenye uwajibikaji unaojenga nidhamu katika mapato na matumizi ya Serikali.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu mpya wa Hesabu za Serikali Prof. Musa Juma Assad akiongea na waandishi wa habari kuhusu  namna atakavyotekeleza majukumu yote yaliyoainishwa katika ofisi yake kwa mujibu wa sheria.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu mpya wa Hesabu za Serikali Prof. Musa Juma Assad (aliyeshika maua) akipongezwa na ndugu, jamaa na marafiki mara baada ya kuapishwa leo. Kulia ni aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali aliyestaafu utumishi wa umma kwa mujibu wa sheria Bw. Ludovick Utouh. (Picha zote na Aron Msigwa –MAELEZO)                                        

No comments:

Post a Comment