Mkuu
wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa Vodacom Tanzania Upendo
Richard(kulia)akimfafanulia jambo kuhusiana na simu aina ya Vodafone smart
kicka Mbunge wa jimbo la
Chalinze mkoani Pwani Mh. Ridhiwani Kikwete (katikati) mara baada ya kuzindua duka jipya la Vodacom Tanzania
lililopo Chalinze mjini Mkoa humo,Kushoto ni Meneja Uhusiano
wa Umma wa kampuni hiyo Matina Nkurlu.
Mbunge wa jimbo la Chalinze mkoani Pwani Mh. Ridhiwani
Kikwete wapili kutoka kulia ,akigonganisha glasi za mvinyo na
baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania ikiwa ni ishara ya kusherehekea
uzinduzi wa duka jipya la kampuni hiyo alilolizindua lililopo Chalinze mjini
Mkoa humo. Hafla hiyo imefanyika leo mkoani humo.
Mkuu
wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa Vodacom Tanzania Upendo
Richard(kushoto)akimfafanulia jambo Mbunge wa jimbo la Chalinze mkoani Pwani
Mh. Ridhiwani Kikwete (kulia) alipofika kuzindua duka jipya la Vodacom Tanzania
lililopo Chalinze mjini Mkoa humo,Kulia kwa Mheshimiwa
ni Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Matina Nkurlu.
Duka
jipya la Vodacom Tanzania lililopo Chalinze mjini Mkoa wa Pwani.
Mbunge wa jimbo la
Chalinze mkoani Pwani Mh. Ridhiwani Kikwete wanne toka kulia akiwa kwenye
picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania,baada ya kuzindua duka jipya la kampuni
hiyo lililopo Chalinze mjini Mkoani humo.
Na Mwandishi wetu, Pwani
4.12.2014
MBUNGE wa jimbo la Chalinze mkoani Pwani Mh. Ridhiwani
Kikwete,ametoa ushauri kwa Makampuni ya Mawasiliano kufungua zaidi vituo vya kutoa huduma
kwa wateja mkoani Pwani na maeneo mengine ya miji midogo inayokua kwa kasi ili
kuwawezesha wateja wake kupata huduma kwa karibu badala ya kuzifuata mbali na
kupoteza muda mwingi ambao wangeutumia kufanya shughuli za uzalishaji.Alitoa
ushauri huo wakati akifungua duka la Vodacom Tanzania lililopo Chalinze mjini ambapo pia alitoa pongezi kwa
hatua hiyo.
Katika kuhakikisha wakazi
wa vitongoji vya Chalinze na maeneo jirani ya Ruvu, Miono, Gwata wanapata
huduma kwa karibu, Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania leo imefungua duka
jipya katika eneo la Chalinze.
Chalinze ni moja ya
kituo maarufu katika mkoa wa Pwani ambacho wanapitia wasafiri wengi
wanaotumia barabara ya Morogoro pia ni makutano ya barabara ya kuelekea mikoa
ya Kaskazini ya Moshi,Tanga na Arusha.Vilevile mji huu unakuwa kwa kasi
kutokana na kuongezeka kwa wafanyabiashara wanaowekeza eneo hili.
Duka hili jipya lenye
mazingira rafiki kwa wateja litakuwa linatoa huduma mbalimbali kwa wateja wa
Vodacom ikiwemo huduma kwa mawakala wa M Pesa na uuzaji wa bidhaa
za Vodacom na litawawezesha wateja wa Chalinze na vitongoji
vyake wakiwemo wasafiri wanaoelekea mikoa mballimbali na nje
ya nchi kupata huduma bora.Mtandao wa Vodacom unaongoza kwa kupatikana vizuri
na umeenea sehemu zote katika mkoa wa Pwani.
Mkuu wa Idara ya Uuzaji na
usambazaji bidhaa wa Vodacom Tanzania Upendo Richard wa Vodacom Tanzania, alisema ufunguzi wa
duka hili la kisasa ni mwendelezo wa malengo ya Vodacom kuendeleza
kuboresha maisha murua kwa kila mtanzania kwa kupata huduma za kampuni
hiyo zenye ubora na kuwafikia wateja kwa urahisi zaidi popote pale walipo
ikiwemo huduma mpya ya kilimo klabu inayolenga kuwawezesha wakulima
nchini.
“Uzoefu na utafiti
umetuonyesha kuwa wananchi wanataka ubora,kama mtandao unaoongoza nchini
tumejizatiti kuhakikisha tunafanya ubunifu wa hali ya juu wa kiteknolojia ili
kutumia mtandao wa simu kuboresha maisha ya wananchi ikiwemo kutoa huduma bora
na ndio maana tunazidi kufungua maduka kama haya kwa ajili ya kuwasogezea karibu
wananchi huduma bora,na ninawahakikishia kuwa popote wateja wetu walipo
tutawafikia na tunawashukuru sana wateja wetu kwa kutuunga mkono na
tunawakaribisha ambao hawajajiunga na familia ya Vodacom kujiunga na kupata
huduma bora kwa gharama nafuu.”Anasema Richard.
Vodacom ina mtandao wa maduka 85 na wakala mbalimbali wakuuza bidhaa zake
nchini na duka lililofunguliwa leo ni la 3 kufunguliwa katika mkoa wa Pwani.
No comments:
Post a Comment