Mkurugenzi wa Wateja wakubwa, Taasisi na Mashirika ya benki ya CRDB, Philip Alfred (kushoto), akiwakabidhi viongozi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Yohana (St. John's) cha mjini Dodoma, mfano wa hundi ya shilingi mil. 10 kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya chuo hicho kilichopo chini ya kanisa la Anglican Tanzania.
Wahitimu wa Shahada ya Sayansi katika Uuguzi wakila kiapo cha utumishi uliotukuka wakati wa mahafali ya tano ya Chuo Kikuu cha St. John's, kinachomilikiwa na kanisa la Anglican kilichopo mjini Dodoma leo.
Meneja wa CRDB Tawi la Dodoma, Bi. Rehema Hamisi akiwa na mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 kwa ajili ya kuikabidhi kwa viongozi wa Chuo Kikuu cha St. John's kama mchango wa
maendeleo ya chuo hicho.
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Philip Alfred aliyekuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya tano ya wanafunzi wa chuo hicho, mjini Dodoma akihuwahutubia wahitimu wa kozi mbalimbali wa chuo hicho.
Mkuu wa Chuo Kikuu Kikuu cha St. John, Askofu Dolnad Mtetemela (katikati), akiwa na viongozi wa kanisa la Anglikan ambalo ndilo mmiliki wa chuo hicho, walipokuwa kwenye mahafali hayo ya tano.
Mkuu wa Shule za Kidini akihutubia jambo kwenye mahafali hayo.
Baadhi ya wandishi wa habari mjini Dodoma, wakimpongeza kwa kumpa maua mwandishi wa gazeti la Mwananchi mkoani humo, Israel Mgusi baada ya kuhitimu shada ya Theogia na Elimu katika chuo hicho.
Wahitimu wa kozi mbalimbali katika Chuo Kikuu cha St. John's wakiwa katika mahafali ya tano ya chuo hicho, yaliyofanyika mjini Dodoma leo.
Wahitimu wa kozi mbalimbali katika Chuo Kikuu cha St. John's wakiwa katika mahafali ya tano ya chuo hicho, yaliyofanyika mjini Dodoma leo.
Wahitimu wa kozi mbalimbali katika Chuo Kikuu cha St. John's wakiwa katika mahafali ya tano ya chuo hicho, yaliyofanyika mjini Dodoma leo. (Picha zote na John Banda)











No comments:
Post a Comment