Katibu
Mkuu wa UVCCM, Sixtus Mapunda, akihutubia katika moja ya mikutano yake.
KATIBU Mkuu wa jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Ndugu Sixtus Mapunda anategemea kufanya ziara ya
siku na nne (14) katika mikoa minne ya Kanda ya Ziwa, ambayo ni Tabora,
Shinyanga, Geita na Kagera kuanzia kesho tarehe 12st Dec 2014.
Ziara
hii ya kikazi ya Katibu Mkuu inalenga kukagua na kuhimiza ujenzi na uimara wa
jumuia ya Vijana katika maeneo husika lakini pia kushiriki kampeni
zinazoendelea za uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mnamo
tarehe 14th Dec 2014.
Pia,
Katibu Mkuu anatarajia kufanya mikutano ya ndani na viongozi wa Jumuiya na
Chama, pia kufanya mikutano ya hadhara
inayolenga kuingiza wanachama wapya ndani ya jumuiya na chama kwa ujumla.
Kuhimiza
wanachama wa chama cha mapinduzi na viongozi kuwaandaa wananchi katika kuipigia
kura katiba mpya iliyopendekezwa wakati ukifika.
Ziara
hiyo ya Katibu Mkuu inategemea kumalizika tarehe 25th Dec 2014.

.jpg)
.jpg)
No comments:
Post a Comment