TANGAZO


Friday, December 5, 2014

Kamati ya Muda ya Wanabloga Tanzania yaanza kupitia Rasimu ya Katiba yao


Mwenyekiti wa Muda wa Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania (Bloggers), Joachim Mushi (wa pili kushoto), akizungumza wakati akifungua majadiliano kwa wajumbe wa kamati ya muda ya wamiliki wa mitandao ya jamii Tanzania ya kujadili rasimu ya Katiba ya umoja huo Dar es Salaam leo. Majadiliano hayo yameanza jana kujadili rasimu ya katiba kabla ya kuipitisha kwa hatua za usajili wa Chama cha Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania (Bloggers).  Kushoto ni Mjumbe wa Kamati hiyo ya muda kutoka Zanzibar, Othman Maulid.
Katibu Msaidizi wa Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania , Shamim Mwasha (kushoto),akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo wakati wa mapitio ya rasimu hiyo. Kulia ni Mjumbe wa Kamati, Henry Mdimu.
Wajumbe wa kamati wakipitia rasimu hiyo. Kulia ni William Malecela na Mariam Ndabaganga.
 Mwenyekiti wa Muda wa Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania (Bloggers), Joachim Mushi (wa pili kushoto), akizungumza wakati akifungua majadiliano kwa wajumbe wa kamati ya muda ya wamiliki wa mitandao ya jamii Tanzania ya kujadili rasimu ya Katiba ya umoja huo Dar es Salaam leo. Majadiliano hayo yameanza jana kujadili rasimu ya katiba kabla ya kuipitisha kwa hatua za usajili wa Chama cha Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania (Bloggers). Kutoka kushoto ni Mjumbe, Othman Maulid, Katibu Msaidizi wa Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania , Shamim Mwasha,  Henry Mdimu (Mjumbe), Mariam Ndabaganga (Mjumbe) na William Malecela (Mjumbe).
Wajumbe wa kamati hiyo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mkutano wao uliofanyika katika Mgahawa wa MOG Longue, jijini Dar es Salaam leo asubuhi.


Na Dotto Mwaibale,
WAJUMBE wa Kamati ya Muda ya Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania (Bloggers) wameanza vikao vyao kujadili rasimu ya katiba ya umoja huo kabla ya kufanya usajili wa chama chao kitakacho waunganisha wamiliki na waendeshaji wa mitandao hiyo Tanzania.
Akizungumza leo katika vikao hivyo vinavyofanyika jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Muda wa Kamati ya Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania, Joachim Mushi amesema wajumbe waliokutana ni wawakilishi wa wamiliki wa mitandao hiyo kutoka makundi mbalimbali ya waendeshaji hao wa mitandao ya jamii nchini.
Alisema pamoja na mambo mengine wajumbe hao wanatarajia kufanya majadiliano baada ya kuipitia rasimu ya Katiba ikiwa ni kuelekea mchakato wa kupata Katiba ya Chama cha Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania. Alisema masuala mengine ambayo yataongoza mjadala huo ni pamoja na kuangalia muundo wa chama, uendeshaji wake, maadili ya chama kwa wanachama katika utekelezaji kazi zao.
"Kikao hiki kinashirikisha wajumbe wa kamati ambao ni wawakilishi wa makundi mbalimbali ya wamiliki na waendeshaji wa mitandao ya jamii Tanzania na kazi kubwa ambayo wataifanya leo kwa pamoja ni kupitia rasimu ya uumoja wetu. Wajumbe wote walikabidhiwa rasimu hii wiki mbili zilizopita kuipitia wenyewe kabla ya kukutaka katika majadiliano ya leo," alisema Mwenyekiti wa Muda, Mushi.
Aidha aliishukuru Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa mchango wake wa dhati wa kuwaunga mkono Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania hasa katika kipindi hiki cha mchakato kuelekea uundwaji wa chama chao. 

Miongoni mwa wajumbe wa kamati hiyo ya muda waliokutana ni pamoja Shamim Mwasha (Katibu Msaidizi) Khadija Kalili (Katibu), Joachim Mushi (Mwenyekiti), Henry Mdimu (Mjumbe), Mariam Ndabaganga (Mjumbe), William Malecela (Mjumbe), Othman Maulid (Mjumbe-Zanzibar) na Francis Godwin (Makamu Mwenyekiti - Iringa).
Mkutano wa mafunzo wa idadi kubwa ya wawakilishi wa wamiliki wa mitandao ya kijamii nchini (Bloggers) uliofanyika Novemba 11, 2014 jijini Dar es Salaam ulioitishwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania uliibua uundwaji wa Kamati ya Muda ya Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania chini, ambapo kamati hiyo ilipewa jukumu la kupitia rasimu kabla ya kushughulikia usajili wa chama cha jumuia hiyo.
(Imeanadaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

No comments:

Post a Comment