TANGAZO


Friday, December 19, 2014

Jokate, Kampuni ya Rainbow ya China wasaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano wa kibiashara wa dola mil. 8

Kampuni ya Kidoti inayomilikiwa na mrembo Jokate Mwegelo na Kampuni ya Rainbow ya China leo wamesaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano wa kibiashara wa dola mil. 8. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa, akizungumza na Mama wa mrembo Jokate Mwegelo, Bernadetta Nduguru (kulia) na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam, Mariam Kisangi wakati wa hafla ya kusaini mkataba huo jijini leo.
Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (kulia), akizungumza na Wakurugenzi wa Gazeti la Jambo Leo, Beny Kisaka (katikati) na Juma Mabakila, wakati wa mkutano huo.

Jokate na viongozi wa Kampuni wa Rainbow wakiwa tayari kwa ajili ya kusaini mkataba huo.
Jokate na viongozi wa Kampuni wa Rainbow wakiteta jambo kabla ya kusaini mkataba huo.
Jokate akizungumza wakati wa mkutano wa kusaini makubaliano ya kibiashara na viongozi wa Kampuni wa Rainbow kabla ya kusaini mkataba huo.
Baadhi ya wageni waliofika katika sherehe za kusaini makubaliano hayo, wakimsikiliza Jokate wakati alipokuwa akizungumza kabla ya kusaini makubaliano hayo jijini leo.
Baadhi ya wageni na maofisa wa kampuni ya Rainbow wakiwa katika hafla hiyo.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Rainbow ya China, inayojishughulisha na utengenezaji wa bidhaa za urembo, Deng Guoxun, akizungumza kabla ya kusaini makubaliano hayo jijini leo.
Jokate Mwegelo, akimshukuru Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Rainbow ya China, inayojishughulisha na utengenezaji wa bidhaa za urembo, Deng Guoxun, kutokana na hotuba yake.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kidoti, inayojishughulisha na masuala ya mambo ya mapambo ya wanawake, mrembo Jokate Mwegelo (kulia) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Rainbow ya China, inayojishughulisha na utengenezaji wa bidhaa za urembo, Deng Guoxun, wakionesha mkataba wa makubaliano ya kibiashara kati yao, Dar es Salaam leo. Kabla ya kuusaini.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kidoti, inayojishughulisha na masuala ya mambo ya mapambo ya wanawake, mrembo Jokate Mwegelo (kulia) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Rainbow ya China, inayojishughulisha na utengenezaji wa bidhaa za urembo, Deng Guoxun, wakisaini mkataba wa makubaliano ya kibiashara kati yao, Dar es Salaam leo. Kushoto ni  Ofisa Mauzo wa kampuni hiyo, Cherry Wong.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Kidoti, inayojishughulisha na masuala ya mambo ya mapambo ya wanawake, mrembo Jokate Mwegelo (kulia) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Rainbow ya China, inayojishughulisha na utengenezaji wa bidhaa za urembo, Deng Guoxun, wakibadilishana mkataba mara baada ya kusaini.























Na Charity James
NEMBO ya Kidoti inayomilikiwa na Mrembo na mwanamitindo nchini, Joketi Mwengelo imeingia mkataba wa Billion 8 na kampuni ya Rainbow Shell Craft ya nchini China.

Akizungumza Dar es Salaam leo, wakati wa kubadilishana hati za mkataba huo wa ubia Jokate alisema makubaliano hayo ni ya kudumu kampuni hizo mbili zitazalisha bidhaa ambazo zitasambazwa ndani na nje ya nchi.
"Ubia huu unalenga kuiwezesha Kidoti kuweza kupanua wigo wake kibiashara ikitazama kujiweka zaidi katika soko la Afrika Mashariki na kati na kuendelea kuweza kuwafikia wateja wengi zaidi,” alisema Jokate.
Aliongeza kuwa ubia huo utawezesha kujengwa viwanda nchini vitakavyotoa fursa ya ajira kwa vijana pamoja na kuinua uchumi wa nchi.
"Hii ni hatua kubwa ya maendeleo kwangu, kama mnavyojua wakati naanza klujishughulisha na masuala ya urembo, ubunifu na uanamitindo sikufikilia kufikia hatua hii ya kuingiza bidhaa zangu kimataifa," alisema.
Kwa upande wake Mwenyekiti Mtendaji wa Rainbow Shell Craft, Mr. Deng Guoxun alisema kuwa katika kipindi kifupi kijacho, Kidoti itakuwa nembo kubwa Afrika Mashariki.

"Kampuni ya Kidoti imeingia ubia na Rainbow hapa Tanzania ili iweze kuwa bidhaa bora na kupendeza zaidi,"  alisema.
Alisema miaka mitatu ijayo nembo ya Kidoti itakuwa nzuri na kubwa sana ambayo itasambaza bidhaa ndani na nje ya nchi, ambazo zitakuwa zinawapendezesha warembo.

Jokate alisema bidhaa za Kidoti zinabuniwa na wabunifu wa Kitanzania wa kampuni hiyo na Rainbow ikitengeneza kile kilichobuniwa na kwamba tayari zinapatikana kwenye supermarkert za Uchumi.
"Mpango ni kuzifanya zianze kupatikana kwenye soko la Kariakoo ambako tunaamini itakuwa rahisi kwa wananchi wengi kuzipata,” alisema Jokate.
Mwegelo aliibukia kwenye mashindano ya urembo na kutwaa taji la Miss Temeke mwaka 2006 ambapo baadaye mwaka huo, alishika nafasi ya pili kwenye Miss Tanzania. Mbali ya kushika nafasi ya pili, pia alitwaa taji la ubalozi wa Redds na The Citizen.

Amekuwa akifanya shughuli mbalimbali za kisanii, ambapo amewahi kucheza filamu kadhaa nchini, kuimba na kutunga nyimbo za muziki wa bongo fleva, MC katika hafla nyingi kubwa nchini ikiwemo Miss Tanzania mwaka huu. Pia ni mtangazaji wa vipindi maalum vya chanel ya muziki ya Chanel O iliyo ndani ya Dstv yenye makao makuu yake Afrika Kusini.

No comments:

Post a Comment