Afisa wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani
akimpima kiwango cha pombe mwilini dereva wa basi la kwenda mikoani, Steven
Mwakibolo kwa kutumia kifaa maalum wakati wa upimaji madereva ikiwa ni sehemu
ya mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani
inayodhaminiwa na Vodacom Tanzania. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha
Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Rosalynn Mworia, akifuatilia
kwa karibu zoezi hilo lililofanyika leo katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani
cha Ubungo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa
Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia, akimuelimisha dereva wa basi liendalo mkoani
Elias Samu kuhusiana na pete ya kidoleni inayotolewa na Vodacom Tanzania kwa
ushirikiano na jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani yenye ujumbe “Wait To Send” unaohamasisha madereva wa
vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi wakati wakiwa wanaendesha vyombo
hivyo. Zoezi hili lilifanyika leo katika kituo cha mabasi yaendayo mkoani cha
Ubungo jijini Dar es Salaam katika mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani
inayodhaminiwa na kampuni hiyo.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Kamanda
Mohammed Mpinga akiwafafanulia jambo Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na
Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia (kushoto) wajumbe wa
Baraza la Taifa la Usalama Barabarani Hamza Kassongo na Henry M. Bantu wakati wa zoezi la upimaji wa
kiwango cha pombe mwilini kwa madereva wa mabasi yaendayo mikoani lililofanyika
leo katika kituo cha mabasi cha Ubungo jijini Dar es Salaam. Zeozi hilo ni mwendelezo
wa kampeni ya Usalama Barabarani
inayodhaminiwa Vodacom.
Maafisa wa Kikosi cha Usalama Barabarani wakimsomea dereva
wa basi la kwenda mikoani matokeo yake ya vipimo vya kilevi mwilini wakati wa
zoezi la upimaji wa kiwango cha pombe mwilini kwa madereva wa mabasi
lililofanyika leo katika kituo cha mabasi yaendayo mkoani cha Ubungo jijini Dar
es Salaam,anaeshuhudia kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano
wa Umma wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia ambapo kampuni yake ni wadhamini wa
kampeni ya Usalama Barabarani.
Mjumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani Hamza
Kassongo pamoja na maafisa wa Vodacom Tanzania wakionyesha pete zenye ujumbe wa
“Wait to Send” wakati wa zoezi la
upimaji wa kiwango cha pombe mwilini kwa madereva wa mabasi yaendayo mikoani
lililofanyika leo katika kituo cha mabasi cha Ubungo jijini Dar es Salaam ikiwa
ni mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani
inayodhaminiwa na Vodacom Tanzania. Pete hizo ziligawiwa kwa madereva wa
mabasi yaendayo mkoani zikiwa na ujumbe huo unaowakumbusha kusubiri hadi wakiwa
wamesimamisha vyombo hivyo ndipo watumie simu zao za mkononi.
Afisa wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani
akimpima kiwango cha pombe mwilini dereva wa basi la mkoani, Elias Samu kwa
kutumia kifaa maalum wakati wa zoezi la upimaji wa kiwango cha pombe mwilini mwa madereva wa mabasi yaendayo mikoani katika mwendelezo wa kampeni ya Usalama
Barabarani inayodhaminiwa na Vodacom
Tanzania. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa
Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia, akifuatilia kwa karibu zoezi hilo
liliofanyika leo katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo jijini Dar
es Salaam.
No comments:
Post a Comment