Baadhi ya wanafunzi waliohitimu mafunzo yao katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) wakiwa katika maandamano ya mahafali ya 10 ya Chuo hicho yaliyofanyika leo Kampasi ya Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Baadhi ya walimu katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) wakiwa katika maandamano katika mahfali ya 10 ya Chuo hicho yaliyofanyika leo kampasi ya Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Zanzibar (Suza) Dk.Ali Mohamed Shein.
Wajumbe wa Baraza la Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) wakiwa katika maandamano yaliyoandaliwa rasmi katika mahfali ya 10 ya Chuo hicho katika kampasi ya Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja leo ambapo mgeni rasmi akiwa .Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Zanzibar (Suza) Dk. Ali Mohamed Shein.
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Said Bakari Jecha (kushtoto) akifuatana na Viongozi akiwemo Mkuu wa Chuo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) wakati wa maandamano katika mahfali ya 10 ya Chuo Hicho yaliyofanyika leo katika Kampasi ya Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Zanzibar (Suza) Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipoku wa akiteta na Makamu Mkuu wa Chuo Prof Idriss Ahmada Rai wakati wa maandamano katika mahfali ya 10 ya Chuo Hicho yaliyofanyika leo katika Kampasi ya Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Zanzibar (Suza) Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) Makamu Mkuu wa Chuo Prof Idriss Ahmada Rai,Waziri wa Elimu na mafunzo ya Amali Ali Juma Shamuhuna na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dk.Idriss Muslim Hija wakisimama wakati Wimbo wa Taifa Ukipigwa katika mahfali ya 10 ya Chuo yaliyofanyika leo katika Kampasi ya Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Baadhi ya wahitimu katika Mahfali ya 10 ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) waliotunukiwa Stashahada ya Sayansi ya Kompyuta wakiwa katika viwanja vya Mahfali hayo katika kampasi ya Chuo Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ambae pia Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) .
Wazee na watoto ambao wamefika katika viwanja vya mahafali ya 10 ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), wakishuhudia wahitimu wanaotunukiwa Vyeti, Stashahada na Shahada na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) leo, ambaye ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) .
Viongozi waliohudhuria katika Mahafali ya 10 ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) yaliyofanyika leo katika Kampasi ya Chuo Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja (kutoka kushoto), Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dk.Mwinyihaji Makame Mwadini,Katibu Mkuu Kiongozi Dk.Abdulhamid Yahya Mzee na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein ambae pia
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), alipokuwa akiwatunuku
Vyeti,Stashahada na Shahada kwa wahitimu wa fani mbali mbali katika
Mahfali ya 10 ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) yaliyofanyika
leo katika Kampasi ya Chuo Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja
(kushoto) Makamu Mkuu wa chuo Prof Idriss Ahamada Rai.
Baadhi ya wahitimu wa Chuo hicho wakimskiliza Mkuu wa Chuo (hayupo pichani), baada ya kutunuku shahada zao.Baadhi ya wahitimu wa Chuo hicho wakimskiliza Mkuu wa Chuo (hayupo pichani) baada ya kutunuku shahada zao.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akiwatunuku shahada wahitimu wa Chuo hicho katika mahafali ya 10 yaliyo fanyika Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.
Mwanafunzi bora wa mahafali ya 10 Chuoni hapo Najat Zahor Said akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Chuo hicho Dkt. Ali Mohamed Shein.
Mwanafunzi bora Najat Zahor Said ambaye amehitimu Shahada ya Sayansi na Elimu akipongezwa na mmoja wa wageni walikwa kwa kushinda nafasi ya kwanza kati ya wanafunzi 741 walio hitimu masomo yao mwaka huu.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Dkt. Ali Mohamed Shein akiwahutubia wahitimu na wageni walikwa katika Sherehe za Mahafali ya 10 ya Chuo hicho. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Dkt. Ali Mohamed Shein akiambatana na Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Idriss Ahmad Rai wakingia katika uwanja wa mahafali ya 10 ya Chuo hicho. Kampasi ya Tunguu Mkoa Kusini Unguja.
Dk. Shein: Tafiti Vyuo Vikuu zilenge kuleta ufanisi, utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya nchi
Na Said Ameir, Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa utanuzi wa
mitaala, ufundishaji na ufanyaji wa tafiti katika vyuo vikuu hauna budi
kuelekezwa katika kufatuta njia na mbinu
za kusaidia kuleta ufanisi katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya nchi.
Akizungumza katika
mahafali ya kumi ya chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) leo, Dk. Shein
amebainisha kuwa lengo la vyuo vikuu hasa vya umma ni kutoa taaluma inayosadia kusukuma
gurudumu la maendeleo ya nchi hivyo shughuli za vyuo hivyo ni lazima zijielekezwe
katika kufanikisha jukumu hilo la kitaifa.
Kwa hivyo alisisitiza
kuwa tafiti katika vyuo hivyo hazina budi zijikite katika kutafuta majibu ya
changamoto za maendeleo katika nchi badala ya kuwa ni njia tu ya kujijengea sifa
za kitaaluma kwa watafiti hao bila ya kujali faida ya tafiti hizo kwa jamii.
Sambamba na kufanya
tafiti Dk. Shein aliongeza kuwa ili tafiti hizo ziweze kuwa na faida kwa taifa
ni lazima kuhakikisha kuwa “matokeo ya tafiti hizo yanafikishwa kwa watafiti
mbalimbali watakaoyatumia matokeo hayo na kuyafanyia kazi”.
Katika mnasaba huo
ameupongeza uongozi wa SUZA kwa kubainisha maeneo maalum ya kipaumbele katika taaluma
na utafiti ambayo yamezingatia mipango ya maendeleo ya nchi na mahitaji ya
jamii.
“hili ni jambo muhimu
kwani kutokana na rasilimali chache tulizonazo hatuwezi kufanya kila kitu, jambo
la busara ni kutafuta maeneo muhimu na tukaweka nguvu zetu katika maeneo hayo”
alieleza Dk. Shein.
Katika hotuba yake
hiyo kwa wahitimu hao, Dk. Shein alisisitiza tena dhamira ya serikali ya kuendelea
kuunga mkono shughuli za utafiti ikiwa ni pamoja na kuongeza bajeti kila hali
ya uchumi inaporuhusu.
Alitumia fursa hiyo kuupongeza
uongozi wa chuo kwa mafanikio iliyopata katika miaka kumi tangu kianze kutoa
wahitimu.
“Ni jambo la kujivunia
hatua kubwa chuo hiki iliyofikia tangu kuanzishwa kwake na kasi ya upanuzi wake
katika kufikia azma ya serikali ya kupata wataalamu wa kutosha kwa nchi yetu” Dk.
Shein alisema.
Alifafanua kuwa
kutoka wahitimu 53 mwaka 2003 kwa programu moja hadi wahitimu 714 kwa programu 12
ni hatua nzuri ya maendeleo ya chuo na kielelezo cha kazi nzuri inayofanywa na
uongozi wa chuo hcho.
Dk. Shein ambaye ni Mkuu
wa Chuo hicho alisifu uamuzi wa uongozi wa chuo kuanzisha programu mbili mpya za
Stashahada ya Ualimu katika Elimu Mjumuisho na Stashahada ya Elimu ya Michezo.
“Nimevutiwa sana na
kuanzisha stashahada ya Elimu ya Michezo na hii inaunga mkono agizo langu la
kutaka kurejeshwa kwa vuguvugu la michezo katika skuli kuanzia msingi hado
vyuoni ili kurejesha heshima ya Zanzibar katika michezo”Dk. Shein alibainisha.
Akizungumza katika
mahafali hayo ambapo jumla ya wahitimu 714 walikabidhiwa vyeti, stashahada na
shahada, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Said Bakari Jecha alisema katika
kukabiliana na changamoto za uendeshaji wa chuo, uongozi umekuwa ukitafuta
ufadhili kwa njia ya kuandika miradi kuimarisha chuo ambapo kwa sasa chuo
kinaendesha miradi 42 iliyo na thamnai
ta dola za kimarekani mil 8.4.
Aliwashukuru wafadhili
mbali mbali wa ndani na nje ya nchi kwa misaada hiyo ambayo inachangia kufanikisha
utekelezaji wa malengo ya mpangokazi wa chuo.
Alitumia fursa hiyo
kuishukuru serikali kwa kuimarisha maslahi ya watumishi wa chuo hicho lakini
akaongeza kuwa bado jitihada zaidi zinahitaji kufanyika katika eneo hilo kwa kuwa
maslahi hayo hasa ya wahadhiri bado ni madogo ikilinganishwa na wenzao Tanzanzia
Bara na nchi jirani.
Wakati
huo huo Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Idris Rai,
alieleza hatua mbali mbali zilizofikiwa na chuo hicho tangu kuanzishwa kwake
mwaka 2001 ambapo kilianza na wanafunzi 53 tu.
Alieleza kuwa
mahafali ya kumi ni tukio la kipekee kwa kuwa yanadhihirisha jitihada kubwa ambazo
zimekuwa zikifanyika kukijenga na kukiimarisha chuo hicho ambacho lengo ni
kukianya kuwa chuo bora katika ukanda huu wa Afrika.
Katika maadhimisho
haya ya miaka kumi chuo hicho imetoa kitabu maalum inachoonesha maendeleo ya
chuo hicho hattua kwa hatua kutoka kuwa na programu moja mwaka 2001 hadi programu
12 mwaka 2014.
No comments:
Post a Comment