Sheikh Abdalla Yussuf Ali alipokuwa akitoa tafsiri ya Quran iliyosomwa na Sheikh Mohammed Juma Issa (hayupo pichani) katika kufungua Mkutano wa Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani za CCM Wilaya ya Mkoani uliohutubiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein katika ukumbi wa Chuo cha Fidel Castro leo akimalizia ziara za kuimarisha Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Pemba.
Wasoma Utenzi Saada Mohamed Zahran na Asha Mohamed Ng’wali wakihani utenzi wao katika wa Mkutano wa Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani za CCM Wilaya ya Mkoani leo uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Fidel Castro chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akimalizia ziara za kuimarisha Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Pemba.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mkoani Omar Makame Haji akimakaribisha Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai wakati wa Mkutano wa Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani za CCM Wilaya ya Mkoani uliofanyika leo katika ukumbi wa Fidel Castro chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akimalizia ziara zake za kuimarisha Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akipokea risala kutoka kwa msomaji Mwanajuma Hassan Kaduara katika wa Mkutano wa Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani za CCM Wilaya ya Mkoani uliofanyika leo katika ukumbi wa Fidel Castro akimalizia ziara zake za kuimarisha Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Pemba.
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani za CCM Wilaya ya Mkoani wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein alipozungumza nao leo katika ukumbi wa Chuo cha Fidel Castro akiwa katika umaliziaji wa ziara za kuimarisha Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Pemba.
Baadhi ya Viongozi na Wazee wa Chama cha Mapinduzi CCM na wajumbe wa Mkutano wa Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani za CCM Wilaya ya Mkoani wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein alipozungumza nao leo katika ukumbi wa Chuo cha Fidel Castro akimalizia ziara za kuimarisha Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Pemba.
Balozi kutoka Jimbo la Makoong’we Bi. Salama Bakari ni miongoni mwa Mabalozi waliotoa michango mbali mbali katika Mkutano wa Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani wa Wilaya ya Mkoani uliofanyika leo katika ukumbi wa Chuo cha Fidel Castro na kuhutubiwa na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohasmed Shein.
Balozi kutoka Jimbo la Makoong’we Bi. Asma Abdalla Abdii ni miongoni mwa Mabalozi waliotoa michango mbali mbali katika Mkutano wa Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani wa Wilaya ya Mkoani uliofanyika leo katika ukumbi wa Chuo cha Fidel Castro na kuhutubiwa na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali MOhasmed Shein.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar alipokuwa akitoa hutuba yake leo kwa kuzungumza na Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani za CCM wa Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba akiwa katika ziara za kuimarisha chama.
Na Ramadhan Othman, Pemba
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein
ameitahadharisha jamii dhidi ya vitendo vya ubaguzi, bugudha na manyanyaso kwa
misingi ya kisiasa na kueleza kuwa vitendo hivyo vinaiangamiza jamii.
Akizungumza
na wananchi wa kijiji cha Maziwang’ombe katika wilaya ya Micheweni Mkoa
Kaskazini Pemba jana, Dk. Shein alisema wananchi ni lazima wazingatie sheria ya
kuanzishwa vyama vingi ambayo imeeleza wazi kuwa kila mwananchi ana haki na
uhuru wa kujiunga na chama chochote cha siasa na kushiriki siasa bila
kubaguliwa.
“tusiwarithishe
chuki wala ugomvi watoto wetu kwani tukiendelea kufanya hivyo tutakuwa
tunaiangamiza jamii yetu ambayo tangu Mapinduzi ya mwaka 1964 ilikuwa ikiishi
kwa amani na upendo” Dk. Shein alisema.
Aliwaeleza
wananchi hao kuwa tofauti za itikadi za kisiasa isiwe kisingizio cha kufanyiana
chuki, kubaguana na kubugudhiana au kutengana kwani watu wote ni ndugu na
wanahitaji kuishi pamoja kwa upendo na kusaidiana.
“Mzazi
atabaki kuwa mzazi, mtoto atabaki kuwa mtoto, ndugu atabaki kuwa ndugu;
inakuwaje tunafanyiana visa na kuhasimiana kwa kuwa tu mwenzetu mmoja ametoka
chama hiki kwenda chama kingine?” aliuliza Dk. Shein.
Dk.
Shein ambaye alifika kijijini hapo kukabidhi boti na mashine ya kisasa yenye
injini ya uwezo wa nguvufarasi 40 kwa kikundi cha Heri ya Moyo Mmoja ambacho ni vijana waliohama chama cha CUF na
kujiunga na CCM.
Vijana hao walifanyiwa visa vya kunyimwa huduma muhimu na hata
kuondolewa katika kazi za pamoja ikiwemo kutengwa katika shughuli za ushirika
ndani ya kijiji hicho.
“kwa
nini wanaotoka katika chama muwabaguwe, muwanyime riziki kwa kuwaondoa katika
ushirika wakati hao ni ndugu zenu na si mahasimu wenu? Mnafanya hivyo kutokana
na siasa za chuki hivyo si sivyo” Dk. Shein aliwaeleza wananchi hao.
Alifafanua
kuwa watu wa Maziwang’ombe hawakuwa na
tabia hiyo na wamekuwa wakiishi kwa upendo katika maisha yao yote kwa
kuheshimiana lakini iweje tangu mfumo wa vyama vingi uliporejeshwa mwaka 1992
wajenga chuki kati yao.
Aliwakumbusha
kuwa vyama vya siasa vinakuja na kupita hivyo hawana budi kuzingatia maisha yao
na kuishi kwa amani na maelewano kama ambavyo viongozi wao wanavyoishi na
kufanya kazi kwa pamoja.
“Mimi
na Maalim Seif hatugombani, hatutukanani. Sijagombana naye wala Mawaziri
wanaotoka katika chama cha CUF, wananiheshimu nami nawaheshimu, tunaheshimiana
na sote tunatekeleza maagizo ya serikali” Dk. Shein aliwaambia wananchi hao
akimaanisha kuwa viongozi hao wanatekeleza majukumu yao katika Baraza la
Mapinduzi bila kuonesha tofauti yeyote.
Aliwaeleza
kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyo chini ya Mfumo wa Umoja wa Kitaifa
haibagui na ndio kiini cha mafanikio iliyoyapata hadi sasa.
“Tunahudumia
wananchi wote bila ya kuangalia itikadi ya mtu na kama tungefanya ubaguzi
tusingefika hapa tulipo” alisema na kuwaeleza watu wa Maziwang’ombe kuwa “
kubaguana si uhodari”.
Aliwataka
wananchi hao kuendelea kushiriki katika shughuli za maendeleo ili kujenga
uchumi wa taifa kwa kufanya kazi kwa bidii na kuwahakikishia kuwa serikali
itaendelea kushughulikia masuala mengine muhimu ya kuendeleza nchi ikiwemo
kuimarisha miundombinu ya bara bara, skuli, hospitali, maji safi na salama,
umeme na mambo mengine makubwa kwa lengo la kuimarisha huduma za jamii.
Hata
hivyo, aliwaasa kutosita kuchangia baadhi ya gharama wanazotakiwa kutoa wakati
wakipata baadhi ya huduma ikiwemo ununuzi wa madaftari kwa watoto wao
wanaokwenda skuli, kutokana na ukweli kwamba idadi ya watu imekuwa ikiongezeka
kwa kasi kubwa kuliko uwezo wa serikali kuweza kumudu mahitaji yao.
Alisisitiza
kuwa hivi sasa serikali haina uwezo tena wa kutoa ajira kwa kila mwananchi na
kuwahimiza kuanzisha vikundi ili serikali iwasaidie na kubainisha kuwa serikali
imedhamiria kuhakikisha kuwa wananchi wanaojikusanya katika vikundi vya
uzalishaji na ushirika wanapatiwa misaada itakayowezesha shughuli za kuwa
endelevu.
“Tupo
hapa kutekeleza ahadi yetu na kusaidia wananchi wenzetu, undeni vikundi vya
kujiajiri, kama mtaendelea kujiunga katika vikundi tutazidi kuwasaidia” Dk.
Shein alisisitiza.
Katika
mkutano huo uliohudhuriwa na mamia ya wananchi wa kijiji hicho na vijiji vya
jirani, Dk. Shein aliwakumbusha wananchi kuzingatia historia yao na kuwahimiza
kudumisha amani na utulivu na kuwatahadharisha dhidi ya kushiriri katika
vitendo vya uvunjifu wa amani kwa kuwa vyombo vinavyohusika na ulinzi na
usalama havitawavumilia.
Wakati
huo huo Waziri wa Ustawi wa Jamii, Uwezeshaji, Vijana, Wanawake na Watoto Bi
Zainab Mohamed Omar aliwahimiza wananchi kujiunga katika vikundi kama
walivyofanya wana kikundi cha Heri ya
Moyo Mmoja ili waweze kufaidika na mpango wa Serikali wa kuwawezesha wananchi
kiuchumi ambao uko chini ya Wizara yake.
Mpango
huo wa kuwawezesha wananchi kiuchumi umelenga kuongeza ajira kwa wananchi
kujiajiri wenyewe kwa kuwa mazingira ya sasa hayaruhusu kila mwananchi kupata
kazi za kuajiriwa serikalini.
Kikundi
hicho kinajumuisha vijana waliokihama Chama cha wananchi (CUF) na kuhamia Chama
cha Mapinduzi (CCM) uamuzi ambao uliwafanya kunyimwa baadhi ya huduma muhimu
kijijini kwao.
Kwa
upande wake Naibu Katibu Mku wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai alihimiza wananchi
kufanya siasa bila ya kubugudhiana au kuwekeana visasi kwa kuwa wakati huo
umepita na kuwataka kufuata nyayo za viongozi wakuu wa vyama vyao ambao
wanafanyakazi pamoja bila ya mivutano.
“viongozi
wetu wakuu wanafanyakazi kwa maelewano makubwa bila mivutano…nasi tufanye hivyo
hivyo tusilete chuki miongoni mwetu na kuumizana na serikali inaonesha mfano
kwa kuleta huduma kwa wananchi bila ya kubagua” alisema Naibu Katibu Mkuu huyo.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi anatarajiwa kumaliza ziara
yake ya siku nne kisiwani humu kwa kuzungumza na viongozi wa mashina na
wenyeviti wa maskani za CCM wa Wilaya ya Mkoani, mkoa wa Kusini Pemba.
No comments:
Post a Comment