Mzunguko wa 14 umekamilika kwa timu zote 20 za ligi kuu ya England kushuka viwanjani.
Chelsea, wameendeleza wimbi la ushindi na kukataa katakata kuzipa nafasi timu nyingine 19 kupunguza pengo la pointi lililopo kati yake na timu hizo.
Chelsea imeendelea kuwa na tofauti ya pointi sita na Man City inayoifuatia baada ya kuirarua Tottenham mabao 3-0, huku Manchester City yenye pointi 30 ikiisasambua Sunderland magoli 4-1. Sergio Aguero ameifungia timu yake ya Manchester City magoli mawili katika mchezo huo, huku Jovetic na Zabaleta kila mmoja akifunga bao moja.
Magoli ya Chelsea yamefungwa na Hazard, Drogba na Remy.
Mchezo mwingine wa Jumatano usiku, ulikuwa kati ya Arsenal na Southampton wanaoshikilia nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu ya England. Mchezaji Alexis Sanchez ndiye aliyekuwa shujaa na kuwanyanyua vichwa mashabiki wa Arsenal pale alipoifungia timu yake goli pekee katika mchezo huo ikiwa ni dakika ya 89 ya mchezo, uliofanyika uwanja wa Emirates na hivyo kujikusanyia pointi tatu muhimu kuelekea kileleni.Arsenal inashikilia nafasi ya sita ikiwa na pointi 23, pointi 13 nyuma ya vinara Chelsea yenye pointi 36.
Everton na Hull City ziligawa pointi baada ya kufungana bao 1-1.
Hadi kufikia mzunguko huo wa 14, Chelsea inaongoza kwa kujikusanyia pointi 36, ikifuatiwa na Man City yenye pointi 30, Southampton ni ya tatu na pointi 26, Huku Manchester United kiwa nafasi ya nne na pointi 25 na nafasi ya tano inashikiliwa na West Ham yenye pointi 24.Ivabaada
No comments:
Post a Comment