Waziri wa mambo ya ndani wa Ivory Coast, Hamad Bakayoko ameahidi kuwa Serikali itashughulikia madai ya maelfu ya Wanajeshi walioandamana.
ametoa ahadi hiyo kwa njia ya Televisheni usiku wa jumanne baada ya Wanajeshi kufunga Barabara katika miji muhimu miwili.
Bayoko amesema Wanajeshi hawatawekewa vikwazo vyovyote kutokana na kuandamana kwao.
Madai ni ya Wanajeshi takriban 9,000 waliokuwa wapiganaji waasi ambao baadae walijiunga na Jeshi.
Wapiganaji hao walikua sehemu ya kikosi kinachomtii Rais Alassane Ouattara aliyechukua madaraka mwaka 2011, na kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Mapema siku ya jumanne,Waziri wa ulinzi Paul Koffi aliwataka Wanajeshi kurejea kambini baada ya kufunga barabara za mji wa Abidjan na Bouake.
Taarifa za jumatano zinasema Wanajeshi tayari wameondoka mjini Bouake.
Haya ni maandamano makubwa kuhusisha jeshi tangu Rais Alassane Ouattara kuchukua madaraka
Mji wa Bouake ni ngome ya Rais wa nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment