TANGAZO


Friday, November 21, 2014

Wakeketaji mashakani Uganda

Jamii ya Sabiny huwakeketa wasichana kuambatana na mila na desturi za jamii hio
Watu watano wakiwemo wanawake na wanaume wamekamatwa na polisi nchini Uganda kutokana na kuwakekeketa wasichana.
Hatua hii si ya kawaida katika nchi ambayo inajaribu kuondoa tabia ambayo wakati Fulani huwa ni ya hatari kwa wahusika.
Watu hao watano wakiwemo wakeketaji walikamatwa katika wilaya ya Kapchorwa ilioko mashariki mwa Uganda ambako tabia hiyo imekithiri.
Wote hao walikiri kosa la ukeketaji ambao ulipigwa marufuku nchini Uganda mwaka wa 2010.
Sheria za Uganda zinachukulia kama kosa sio tu kukeketa lakini pia na yule anaefanya tohara hiyo ama yeyote anaeshiriki katika shughuli yoyote ile inayopelekea kufanya kitendo cha tohara.
Tangu sheria hiyo ipitishwe miaka mitano iliopita kumekuwa na visa vya kukamata wanaoshiriki katika ukeketaji lakini kufunguliwa mashtaka kumekuwa nadra.
Sheria imeleta hofu miongoni ma jamii ya Sabiny ambayo inachukulia ukeketaji kama mila na desturi yao. Hata hivyo kuna wale wahafidhina ambao bado wanafanya tohara kwa wasichana kwa kujificha hususan sehemu za mashambani.
Wanaharakati wanaopiga vita utamaduni huo wanasema kuwa ukeketaji una madhara yake, ikiwemo kuvuja damu pamoja na uwezekano wa kidonda kuambukizwa.
Isitoshe mhusika yaani yule anaekektwa huenda asiweze kuzaa maishani mwake au kupata matatizo wakati wa kujifungua na mara kadhaa mtu huyo huweza kufariki.
Hatua ya Uganda ya kuwafungulia mashataka wakeketaji inakuja siku chache baada ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kuzindua kampeini ya kukomesha ukeketaji duniani.

No comments:

Post a Comment