Mkuu wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa Vodacom Tanzania Upendo Richard (katika), akimfafanulia jambo Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Ahmed Kipozi, kabla ya kuzindua duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo Barabara ya Soko jipya Bagamoyo mjini mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja Masoko wa Kanda ya Pwani Florantina Urio.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Ahmed Kipozi, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo barabara ya soko jipya Bagamoyo mjini mwishoni mwa wiki. Wengine katika picha katikati ni Mkuu wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa Vodacom Tanzania Upendo Richard na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo Rosalynn Mworia.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Ahmed Kipozi (wapili kushoto) akifungua mvinyo (shampeni) kuashiria uzinduzi wa duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo barabara ya soko jipya Bagamoyo mjini mwishoni mwa wiki. Wengine kushoto ni Mmiliki wa duka hilo Simon Mwambapa na kulia ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo Rosalynn Mworia.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Ahmed Kipozi (wapili kushoto), Mkuu wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa Vodacom Tanzania Upendo Richard (kushoto), Mmiliki wa duka hilo Simon Mwambapa (watatu kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Rosalynn Mworia wakigonganisha glasi zenye mvinyo kuashiria ishara ya uzinduzi wa duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo barabara ya Bagamoyo mjini mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Ahmed Kipozi (katikati) akiagana na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia(kulia) mara baada ya kuzindua duka jipya la kampuni hiyo lililopo barabara ya soko jipya Bagamoyo mjini mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa kampuni hiyo Upendo Richard.
Na Mwandishi wetu
Katika kuhakikisha wakazi wa Bagamoyo na maeneo jirani ya Boko
na Bunju wanapata huduma kwa karibu,Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania
mwishoni mwa wiki imezindua duka jipya katika mji wa kihistoria wa
Bagamoyo.
Bagamoyo ni moja ya miji ya kihistoria nchini wenye vivutio
vikubwa vya utalii na ulikuwa kituo kikubwa cha biashara ya utumwa ambapo
watalii wengi hupenda kuvitembelea kila mara pia katika mji huo inajengwa
bandari kubwa inayotarajiwa kufunguliwa hivi karibuni.Vile vile mji huo una
mahoteli na mandhari tulivu inayovutia wananchi wengi kupenda
kuutembelea.
Duka hili jipya lenye mazingira rafiki kwa wateja litakuwa
linatoa huduma mbalimbali kwa wateja wa Vodacom ikiwemo huduma kwa
mawakala wa Mpesa na uuzaji wa bidhaa za kampuni hiyo na litawawezesha
wateja wa bagamoyo wakiwemo wageni wanaotembelea eneo hilo na wateja
kutoka maeneo ya jirani kama Boko na Bunju.Mtandao wa Vodacom
unaongoza kwa kupatikana vizuri na umeenea sehemu zote katika wilaya
hiyo.
Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn
Mwori, alisema ufunguzi wa duka hili la kisasa ni mwendelezo wa malengo
ya kampuni yetu katika kuendeleza kuboresha maisha murua kwa kila
mtanzania kwa kupata huduma za kampuni hiyo zenye ubora na kuwafikia wateja kwa
urahisi zaidi popote pale walipo ikiwemo huduma mpya ya kilimo klabu
inayolenga kuwawezesha wakulima nchini.
“Uzoefu na utafiti umetuonyesha kuwa wananchi wanataka
ubora,kama mtandao unaoongoza nchini tumejizatiti kuhakikisha tunafanya ubunifu
wa hali ya juu wa kiteknolojia ili kutumia mtandao wa simu kuboresha maisha ya
wananchi ikiwemo kutoa huduma bora na ndio maana tunazidi kufungua maduka kama
haya kwa ajili ya kuwasogezea karibu wananchi huduma bora,na ninawahakikishia
kuwa popote wateja wetu walipo tutawafikia”Alisema Mworia.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Ahmed
Kipozi,aliipongeza kampuni hiyo kwa kufungua duka katika eneo hilo lenye
watalii na wananchi wengi na kuongeza kuwa anaamini litawaokolea muda waliokuwa
wanatumia kufuata huduma za Vodacom mbali na kuwasihi kutumia huduma ya M pesa
na M Pawa kwani ni huduma iliyo bora na
yenye usalama zaidi.
Mpaka sasa Vodacom ina mtandao wa maduka 83 na wakala mbalimbali wakuuza
bidhaa zake nchini na duka lililofunguliwa leo ni la kwanza katika wilaya ya Bagamoyo.
No comments:
Post a Comment