Naibu Waziri Malima akiz ungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuifungua semina hiyo. |
Picha ya pamoja ya mkutano huo.
|
Baadhi ya wadau wa semina hiyo wakifuatilia ripoti.
|
Na Magreth Kinabo
TANZANIA imepata alama ya pointi 4.5 katika masuala ya uongozi bora kwenye ripoti ya maendeleo ya ukuaji wa uchumi wa nchi za Afrika(Afrika
For Results) ya mwaka huu.
Hayo yalisemwa leo na
Waziri wa fedha,Adam Malima wakati akizungumza katika ufunguzi wa semina ya siku nne wa kutathimini ripoti
hiyo kwa nchi ya Tanzania
ukilinganisha na tafiti za nchi zingine za Afrika unaoendelea kwenye hoteli ya
Kunduchi Beach jijini Dares Salaam.
“ Katika ripoti hii kipimo cha alama zilizotumika ni 0-5 , hivyo Tanzania imefanya
vizuri katika masuala ya uongozi bora kwa kupata alama hiyo,” alisema Malima.
Katika ripoti
iliyoandaliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika(ABD) ikishirikiana na Serikali ya
Tanzania ambayo imetaja maeneo sita ya kuzingatia katika kuhakikisha ukuaji wa
uchumi unafika kwa wananchi wote
wakiwemo wa kawaida kwa
kuzingatia hilo na mengineo.
Aliyataja maeneo hayo
ambayo ni uwajibikaji
kwa alama 4.1. uwezo wa kitaasisi
alama 4, mikakati ya kibajeti alama
2.9, mipango yenye kuleta matokeo
alama 4.5 na matumizi ya Tehama alama 2.3.
Naibu Waziri huyo alisema
ili kutengeneza fursa sawa katika ukuaji
wa uchumi ni muhimu kuboresha viashiria
vya kukua kwa uchumi na kupunguza umaskini.
“Wananchi wa kawaida wanaambiwa kuwa uchumi umepanda kwa asilimia
saba lakini, baadhi yao hali yao kimaisha
bado ni duni na wanashindwa kuamini
ukuaji huo hivyo kwa kutumia viashilia
hivyo tunaweza kugundua na kuboresha baadhi ya maeneo ambayo yameonekana kuwa
chanzo cha kutowafikia wananchi wa kawaida,”alisema Malima.
Wadau hao katika mkutano
huo watajadili njia ambazo zitakazo saidia kuwafikia wananchi
wa kawaida kukua kiuchumi ili kufikia Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025
ya kuwa nchi yenye uchumi wa kati.
Kwa upande wake
Mwakilishi Mkazi wa ADB, Tonia
Kandiero alisema wadau
hao watajadili ripoti
hiyo katika mkutano huo wa kutathimini ripoti
hiyo kwa nchi ya Tanzania kwa siku nne, na kulinganisha na nchi zingine za Afrika.
Akitoa uzoefu wake
katika nchi ya Zimbabwe, Erick
Zinyengere, ambaye ni Meneja wa Ushauri alisema ili kuweza kuleta
mafanikio ya kimaendeleo katika miradi mbalimbali ni vema kushirikisha wananchi
katika
hatua ya kwanza hadi ya mwisho.
No comments:
Post a Comment