*Litakuwa na urefu wa kilometa 7.5
*Litaanzia eneo la Aghakani na kuishia Coco beach
*Ujenzi kuanza mapema mwakani
Waziri wa Ujenzi Dkt.
John Magufuli akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu
ujenzi wa daraja lenye urefu wa kilometa 7.5 litakaloanzia eneo la Aghakani na
kuishia Coco beach, ujenzi huo unaotarajiwa kuanza mapema mwakani na unafadhiliwa na Serikali ya watu wa Korea Kusini, lengo
ni kupunguza msongamano wa magari katika daraja la Serender.
Waziri wa Ujenzi Dkt.
John Magufuli(kulia),akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es
Salaam kuhusu ujenzi wa daraja lenye urefu wa kilometa 7.5 litakaloanzia eneo
la Aghakani na kuishia Coco beach, ujenzi huo unaotarajiwa kuanza mapema
mwakani na unafadhiliwa na Serikali ya watu wa Korea Kusini ,lengo
ni kupunguza msongamano wa magari katika daraja la Serender,kushoto ni Katibu
Mkuu Wizara ya Ujenzi Dkt. Juma Iyombe. (Picha Lorietha Laurence – Maelezo)
Na Beatrice Lyimo -Maelezo
18/11/2014
Zaidi ya Bilioni 110 zinatarajia kutumika katika ujenzi wa daraja lenye urefu wa kilometa 7.5 ili kupunguza msongamano wa magari jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli alisema daraja hilo litaanzia eneo la Aghakani na kuishia Coco beach.
Waziri Dkt. Magufuli alisema daraja hilo litakalojengwa kwa msaada wa Serikali ya Korea Kusini litakuwa na njia nne na barabara mbili za huduma kwa kila upande lenye uwezo wa kupitisha magari elfu 61 kwa siku .
“Serikali ya Korea Kusini imemaliza mradi wa ujenzi wa daraja la Kikwete pamoja na barabara ya Malagalasi Mkoani Kigoma na sasa tumewaomba waendelee kutoa msaada kwa ajili ya ujenzi wa barabara mkoani Dar es Salaama ili kupunguza msongamano wa magari”, alisema Dkt. Magufuli.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu kutoka TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale amebainisha kuwa wataalamu kutoka Korea Kusini wameshafanya Upembuzi yakinifu uliomalizika hivi karibuni, hivyo ujenzi wa daraja hilo unatarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwaka ujao.
Aliongeza kuwa daraja hilo litakalofahamika kwa jina la New Salender Bridge litaunganishwa na barabara ya Ally Hassan Mwinyi kutokea Aghakani na kwa upande mwingine litaunganishwa na barabara ya Chole iliyopo Masaki.
Serikali imeweka mikakati mingi ya kupunguza msongamano wa foleni za magari kwa kuanzisha ujenzi mbadala wa barabara za juu unaotarajiwa kujengwa maeneo ya TAZARA,Mbagala rangi tatu hadi gerezani, kuanzishwa kwa kivuko cha Dar es Salaam hadi Bagamoyo.
Pia utafanyika utanuzi wa barabara nyingine za Dar es salaam kwenda Morogoro kupitia Chalinze na ile ya Morocco hadi Mwenge na Bagamoyo hadi Msata.
No comments:
Post a Comment