TANGAZO


Saturday, November 15, 2014

Rais wa Algeria alazwa hospitalini

Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika akitembea kwa kutumia kiti cha magurudumo.kiongozi huyo wa miaka 77 adaiwa kulazwa katika hospitali moja nchini Ufaransa.
Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika amelazwa katika hospitali moja nchini Ufaransa.
Kulingana na maafisa wa Ufaransa kiongozi huyo ambaye aliugua kiharusi mwaka uliopita kwa sasa anapata matibu katika mji wa Gronoble maafisa wa serikali na polisi wamesema.
Maafisa hao hatahivyo hawakutoa maelezo zaidi kuhusu afya ya Bouteflika.
Bouteflika mwenye umri wa miaka 77 na ambaye ameiongoza Algeria tangu mwaka 1999 amekuwa haonekani hadharani tangu achaguliwe kwa muhula wake wa nne mamlakani mnamo mwezi Aprili.
Rais Abdelaziz Bouteflika kushoto
Gazeti la kijimbo Le Dauphine Libere limesema kuwa Bouteflika alilazwa katika kitengo cha kukabiliana na magonjwa yamoyo katika mji wa kusini mashariki mwa Ufaransa.
Gazeti hilo limesema kuwa vyumba vyote katika ghorofa alikolazwa vilichukuliwa ili kuimarisha usalama.
Hatahivyo serikali ya Algeria haijatoa tamko lolote kuhusu ripoti ya rais huyo kulazwa.
Kiongozi wa chama tawala cha FNL hatahivyo amekana ripoti hizo.

No comments:

Post a Comment