Katibu,
Ofisi ya Rais Sekretariet ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Exavier Daudi
(kushoto) akimkaribisha ofisini kwake Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO)
Bw. Assah Mwambene wakati alipotembelea ofisi hiyo kwa lengo la kuangalia
utendaji kazi wa kitengo cha mawasiliano.
Katibu,
Ofisi ya Rais Sekretariet ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Exavier Daudi akimueleza
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene kuhusu mikakati ya
ofisi hiyo ya kuboresha mawasiliano ya serikali kwa umma wakati wa ziara ya
Mkurugenzi wa Idara ya Habari katika vitengo cha mawasiliano.
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene (kushoto) akizungumza na
Katibu, Ofisi ya Rais Sekretariet ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Exavier
Daudi wakati alipotembelea ofisi hiyo ikiwa ni utekelezaji wa mkakati wa Idara
ya Habari kutembelea vitengo vya mawasiliano kwenye taasisi za serikali ili
kuangalia utendaji kazi wa vitengo hivyo.
Ofisa
Habari wa Ofisi ya Rais Sekretariet ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Kassim
Nyaki (kulia) akieleza kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah
Mwambene kuhusu mafanikio ya kitengo cha mawasiliano cha ofisi hiyo katika kutoa taarifa kwa umma ambapo alisema
hadi sasa tovuti yao ina zaidi ya watu Elfu 8 wanaotembelea kwa siku.
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene (kulia mwenye Kaunda Suti)
akiwaeleza baadhi ya viongozi wa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii katika kuboresha mawasiliano ya
serikali kwa umma. Katikati ni Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali Bw. Francis Mwakapalila.
Kaimu
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bw. Francis Mwakapalila (kulia)
akifurahia jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene
wakati alipotembelea Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
ili kujionea utendaji kazi wa kitengo cha mawasiliano serikalini. Katikati ni
Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa ofisi hiyo Bw. Gerard
Mwanilwa.
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene (kulia) akisisitiza kwa Maafisa Habari wa Ofisi ya Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu utoaji wa taarifa kwa umma kwa wakati. Kushoto ni Ofisa Habari wa Ofisi
hiyo Bi. Evelyne Thomas. (Picha zote na Fatma Salum-MAELEZO)
No comments:
Post a Comment