Mabingwa watetezi wa kombe la Afrika Nigeria wameicharaza Congo Brazaville 2-0 siku ya jumamosi ili kuimarisha matumaini yake ya kufuzu katika dimba la Afrika mwaka 2015 huku Afrika kusini na Cameroon zikifuzu katika kinya'nganyiro hicho.
Afrika kusini iliichapa Sudan 2-1 katika mechi yao ya kwanza tangu kuuawa kwa mlinda lango wake Senzo Meyiwa ili kuongoza kundi la Da.
Zambia nayo iliinyamazisha Mozambique 1-0 mjini Moputo kufuzu na katika kundi Fa pamoja na viongozi wa kundi hilo Cape Verde.
Burkina Faso na Gabon pia zilifuzu katika kundi Cha baada ya Kuishinda Lesotho 1-0 mjini Maseru huku Angola ikipata sare ya bila kwa bila dhidi ya wenyeji wake mjini Luanda.
Siku ya Ijumaa Tunisia ilitoka sare ya bila kwa bila na Botswana na hivyobasi kufuzu katika fainali hizo.
Kwengineko mabao mawili ya kipindi cha pili ya Ikechukwu Uche na Aaron Samuel dhidi ya Congo katika mji wa Pointe-Noire yaliimarisha matarajio ya Nigeria kufuzu katika fainali za kombe hilo.
Mjini kampala,Uganda iliiadhibu Black Stars ya Ghana 1-0 baada ya timu zote mbili kupata sare ya moja kwa moja mjini kumasi miezi mitatu iliopita.
Bao la ushindi la Uganda liliwekwa wavuni na Savio kabugo ambaye alifunga bao hilo baada ya dakika 10 pekee.
No comments:
Post a Comment