TANGAZO


Monday, November 17, 2014

Madaktari wamuua mshukiwa wa wizi India

Hospitali maarufu ambako mauaji hayo yalifanyika
Polisi nchini India wanasema kuwa kikundi cha madaktari kimempiga hadi kufa mshukiwa wa wizi katika taasisi ya mafunzo ya udaktari mjini Calcutta mashariki mwa India.
Mwanamume huyo alifungwa kwenye mlingoti na kucharazwa viboko huku uume wake ukikatwakatwa kwa wembe.
Polisi wanasema kuwa mshukiwa huyo alidaiwa kuiba simu za mkononi. Watu wawili wamezuiliwa na polisi huku uchunguzi ukiendelea kufanywa.
Wandishi wa habari wanasema kuwa mauaji hayo ni dalili ya tatizo la watu kuwaadhibu washukiwa wa uhalifu nchini India hadharani.
Lakini kinachoshangaza sana katika tukio hili ni kuhusika kwa madaktari katika kitendo hicho.
Madaktari hao walimburura mwanamume huyo hadi katika chumba kimoja cha hospitali hiyo na kuanza kumshambulia kabla ya kumuacha akiwa hali mahututi ambapo baadaye alifariki.
Baadhi ya madaktari walimshambulia mwanamume huyo katika sehemu zake za siri na kumkatakata kwa wembe kitendo amabcho kimewashtua wengi.

No comments:

Post a Comment