Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein (kulia) akifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Magharibi CCM Yussuf Mohammed Yussuf (katikati) na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai mara alipowasili katika Tawi la Chuo cha Mwalimu Nyerere Bububu Kihinani Mkoa wa Magharibi Kichama nje ya Mji wa Unguja kuzungumza na Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani wa Wilaya ya Mfenesini katika kuimarisha Chama.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein (katikati) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai (kulia) Mwenyekiti wa Wilaya ya Mfenesini Kichama Mjumbe Msuri wakiwa katika ukumbi wa Tawi la Chuo cha Mwalimu Nyerere Bububu Kihinani Mkoa wa Magharibi Kichama nje ya Mji wa Unguja katika mkutano maalum wa kuimarisha Chama kwa Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto) akitia saini kitabu cha wageni alipofika katika ukumbi wa Tawi la Chuo cha Mwalimu Nyerere Bububu Kihinani Mkoa wa Magharibi Kichama nje ya Mji wa Unguja kuzungumza na Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani Wilaya ya Mfenesini katika kuimarisha Chama. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai (kulia) wakati wa mkutano wa maalum wa kuimarisha Chama cha Mapinduzi CCM kwa Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani Wilaya ya Mfenesini CCM.
Balozi wa Shina namba 36 Jimbola Mtoni Abdul-Aziz Salum akisoma risala ya Mabalozi wa Wilaya ya Mfenesini Kichama mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein alipokuwa Mgeni rasmi katika Mkutano Maalum kwa Viongozi hao akiwa katika ziara zake za kuimarisha Chama katika Mikoa ya Unguja.
Mkuu wa Tawi la Chuo cha Mwalimu Nyerere kiliopo Bububu Kihinani Prof Shadrack Mwakalika akitoa shukurani zake leo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein alipofika chuoni hapo kuzungumza na Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani Wilaya ya Mfenesini CCM katika ziara maalum za kuimarisha Chama katika Mikoa ya Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akizungumza na Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani katika ukumbi wa Tawi la Chuo cha Mwalimu Nyerere Bububu Kihinani Mkoa wa Magharibi Kichama akiwa katika ziara zake za kuimarisha Chama cha Mapinduzi CCM katika Wilaya ya Mfenesini.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akizungumza na Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani katika ukumbi wa Tawi la Chuo cha Mwalimu Nyerere Bububu Kihinani Mkoa wa Magharibi Kichama akiwa katika ziara zake za kuimarisha Chama cha Mapinduzi CCM katika Wilaya ya Mfenesini.
Balozi kutoka Jimbo la Dole, Abdalla Juma Abdalla akitoa mchango wake wakati wa Mkutano wa Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani za CCM Wilaya ya Mfenesini uliohutubiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein leo katika Ukumbi wa Tawi la Chuo cha Mwalimu Nyerere Bububu Kihinani, Mkoa wa Magharibi.
Baadhi ya Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani katika Wilaya ya Mfenesini Kichama wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akizungumza na Viongozi hao katika Ukumbi wa Tawi la Chuo cha Mwalimu Nyerere Bububu Kihinani Mkoa wa Magharibi akiwa katika ziara zake za kuimarisha Chama cha Mapinduzi CCM Mikoa ya Unguja.
Na Said Ameir, Zanzibar
Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amewahakikishia
wananchi kuwa Serikali itaendelea kuchukua hatua za haraka shughulikia matatizo
ya ardhi katika mashamba ya Selemu, Dole na Ndunduke katika wilaya ya Magharibi
lakini kwa utaratibu unaozingatia sheria ya Ardhi ya Zanzibar.
Aliwakumbusha wananchi
kuwa sheria ya ardhi inatamka wazi kuwa ardhi yote ni mali ya serikali hivyo wananchi
waliomilikishwa ardhi hiyo wanapaswa kutii sheria na masharti yanayoambatana na
sheria hiyo kuhusu matumizi ya ardhi husika.
Dk. Shein ametoa
kauli hiyo leo wakati akizungumza na viongozi wa mashina na maskani za Chama
cha Mapinduzi wilaya ya Kichama ya Mfenesini Mkoa wa Magharibi katika siku yake
ya nne ya kutembelea viongozi hao katika wilaya zote za Unguja na Pemba.
“baadhi ya wananchi waliopata
mashamba ya eka tatu wanayagawa viwanja, hii ni kinyume na sheria. Sisi tutalishughulikia
tatizo hili kwa kufuata sheria na ikibidi tutafuta milki za baadhi ya watu hao”
Dk. Shein alisisitiza.
Katika risala ya
viongozi hao pamoja na baadhi ya waliopata fursa ya kuzungumza katika mkutano
huo walieleza tatizo la ardhi katika maeneo hayo hasa suala la baadhi ya mashamba
hayo kugeuzwa maeneo ya makazi kinyume na matumizi yaliyokusudiwa.
Katika mkutano huo
uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
nje kidogo ya mji wa Zanzibar, Dk. Shein alieleza tangu kuingia madarakani
amekuwa akiendesha serikali kwa kufuata Katiba na Sheria na kuongeza kuwa yeye
si mgeni katika kuendesha serikali.
Alibainisha kuwa
mambo yote yanayotekelezwa na serikali hiyo yanafanyika kwa makubaliano likiwemo
suala la Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambalo lilipitia hatua zote katika
serikali na kutekelezwa kwa mujibu wa sheria hiyo hivyo haoni sababu kujitokeza
mtu akasema serikali hiyo inaendeshwa kibabe.
“Mimi si mgeni katika
uongozi nimepitia ngazi mbalimbali kuanzia Naibu Waziri, nimekuwa Waziri kamili,
Makamu wa Rais na kufanya kazi na Marais wa wawili kwa mafanikio hadi leo
nimekuwa Rais wa Zanzibar hivyo si mgeni katia kuongoza nchi” Dk. Shein
alieleza.
Aliongeza kuwa
kutokana na uongozi wake bora na makini, viongozi mbalimbali wanaofika nchini
wamekuwa wakisifu uongozi wake na serikali kwa jumla kwa kuimarisha amani na utulivu
ambao umesaidia serikali kutekeleza majukumu yake ya kuwaletea wananchi
maendeleo.
Matokeo yake alieleza
Serikali imekuwa ikitekeleza vyema Ilani ya uchaguzi ya CCM kwa hivyo anaamini
kuwa wananchi wataendelea kukichagua chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao.
Kwa upande wake Naibu
Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai akimkaribisha Dk. Shein alieleza
kuwa kumekuwepo na jitihada za makusudi za kupotosha wananchi juu ya Katiba
Iliyopendekezwa kwa baadhi ya watu kueleza vitu ambavyo havihusiani na Katiba
hiyo.
“Tulikwenda katika Bunge
Maalum la Katiba kuzungumzia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wala sio
Katiba ya Zanzibar lakini wao wanaeleza mambo ambayo yanayopaswa kuzungumziwa na
wananchi wa Zanzibar wenyewe wakati wa watakapozungumzia Katiba yao ya Zanzibar”
alisema Naibu huyo huku akitolea mfano suala la ardhi.
Mkutano huo
ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho wakiwemo wajumbe wa Kamati
Kuu pamoja na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM.
Dk. Shein anatarajiwa
kuendelea na ziara yake kesho kwa kutembelea wilaya ya Kati.
No comments:
Post a Comment