Kundi la wanaharakati wanaopigania demokrasia katika eneo la Hong Kong wameandamana hadi katika makao rasmi ya kiongozi mkuu wa Hong Kong, ili kuonyesha hasira zao dhidi ya matamshi aliyoyatoa kuhusiana na watu maskini nchini humo .
Katika mahojiano, CY Leung alionekana kuashiria kwamba kuwapa watu maskini kura sio jambo jema .
Waandamanaji bado wako barabarani licha ya mazungumzo ya jana kati ya viongozi wa wanafunzi na maafisa wa serikali.
Waandamanaji hao wanawataka viongozi wa China kuikubalia Hong Kong kuandaa uchaguzi huru na wa haki.
Mmoja wa waandamanaji , Jeffrey Chang, anasema ni thibitisho kuwa CY Leung amevuka mpaka
No comments:
Post a Comment