TANGAZO


Monday, October 6, 2014

Umaskini bado jinamizi duniani

Shinikizo limetolewa kwa viongozi wa mataifa duniani kumaliza kiwango kikubwa cha umasikini duniani
Shirika linalopiga vita umasikini duniani la (ONE Campeign ) limetoa wito kwa serikali za dunia kuafikiana kuhusu mpango wa kukabiliana na viwango vikubwa vya umaskini ifikapo mwaka 2030.
Kampeini hiyo mpya itachukua nafasi ya mradi wa kufanikisha malengo ya mileni unaomalizika mwaka ujao.
Katika ripoti yake ya kila mwaka, kundi hilo linasema katika baadhi ya mataifa yaliopo Kusini mwa jangwa la sahara bado kuna tatizo kubwa la serikali kutumia kiwango kidogo sana cha pesa kupambana na umasikini na kwamba tatizo hili ni sugu ila linahitaji kutatuliwa.
Pia kundi hilo linasema ufadhili mkubwa bado utahitajika kusaidia juhudi hizo dhidi ya umasikini.
Ripoti hiyo inasema kwamba mataifa yamo katika njia panda katika kukabiliana na umaskini. Kumekuwa na jitihada nyingi Katika sehemu nyingi. Lakini maendeleo ya siku zijazo, yanatishiwa, kutokana na ukosefu wa usawa, ukosefu wa ajira na jitihada zilizositishwa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Kundi hilo linasema kuwa wafadhili wengi wanashindwa kulenga na kutoa misaada kwa nchi zilizo maskini Zaidi na zilizomo kwenye hatari.
Ripoti hiyo pia inasema serikali nyingi za Kiafrika hazitimizi ahadi zao za matumizi katika sekta muhimu kama vile za afya, kilimo na elimu.
Ripoti ya ONE inasema mwaka ujao wakati malengo mapya yatatangazwa ya kukabiliana na umaskini wa hali ya juu na maamuzi yatakapo chukuliwa kuhusu ufadhili wa kuyafikia malengo hayo, huenda yakatoa nafasi murwaa na ya kihistoria kwa mataifa hayo.

No comments:

Post a Comment