TANGAZO


Monday, October 6, 2014

Uchaguzi kuingia duru ya pili Brazil

Roussef akosa kupata kura za kumwezesha kutangazwa rais
Huku zaidi ya asilimia 97 ya kura zilizopigwa zikiwa zimehesabiwa kwenye uchaguzi mkuu nchini Brazil, rais Dilma Roussef ameshinda awamu ya kwanza ya kura hizo, lakini bado hajapa ushindi unaohitajika ili kuzuia kuwepo duru ya pili.
Mpinzani wake wa karibu Aecio Neves amechukua nafasi ya pili.
Matokeo haya hata hivyo yanamaanisha kuwa mgombea mwingine ambaye ni waziri wa zamani wa mazingira Marina Silva ameondolewa kwenye kinyanganyiro hicho hata baada ya kuonekana kuwa kwenye nafasi nzuri ya kuwa rais wa Brazil.
Takriban watu milioni 150 walipiga kura katika uchaguzi wa saba wa nchi hiyo tangu kumalizika kwa utawala wa kijeshi mwaka 1985.
Heka heka za uchaguzi Brazil
Bi Rousseff aliendesha kampeni yake akitumia rekodi yake ya kubuni programu ambazo zimesaidia kukwamua mamilioni ya watu kutoka umaskini nchini Brazil.
Cha kushangaza zaidi katika uchaguzi huu ni dalili ya kupoteza uungwaji mkono kwa waziri wa zamani wa mazingira Marina Silva.
Mwezi mmoja uliopita Bi Silva alikuwa aking'aa kwenye kura ya maoni baada ya kuchukua usukani kama mgombea wa urais kupitia kwa chama cha Kisoshiolisiti kufuatia kuaga dunia kwa mgombea mwenza kwenye ajali ya ndege.
Lakini mijadala yake isiyo ya kuridhisha na pia uamuzi wa wapiga kura wa kutotaka kupigia kuya vyama vya zamani ina maana kuwa Bi Silva amendoka kabisa kwenye kinyanganyiro hicho.

No comments:

Post a Comment