Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Angellah
Kairuki akitoa mada wakati wa mkutano wa Umoja wa Wabunge Wanawake kuhusu maandiko ya kisera na manufaa
waliyopata wanawake katika Rasimu ya mwisho ya Katiba inayopendekezwa uliofanyika
mjini Dodoma leo 3 Septemba, 2014.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Anna Abdalah
akitoa mada wakati wa mkutano wa Umoja wa Wabunge Wanawake kuhusu maandiko ya
kisera na manufaa waliyopata wanawake katika Rasimu ya mwisho ya Katiba
inayopendekezwa uliofanyika mjini Dodoma leo 3 Septemba, 2014.
Mhadhiri Msaidizi wa Sheria katika Chuo Kikuu cha
Iringa, Bw. Dunford Mpelumbe akitoa mada wakati wa mkutano wa Umoja wa
Wabunge Wanawake kuhusu maandiko ya
kisera na manufaa waliyopata wanawake katika Rasimu ya mwisho ya Katiba
inayopendekezwa uliofanyika mjini Dodoma leo 3 Septemba, 2014.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Dkt. Mary
Mwanjelwa akitoa neno la shukurani mara baada ya kumalizika kwa utoaji mada
kuhusu maandiko ya kisera na manufaa waliyopata wanawake katika Rasimu ya
mwisho ya Katiba inayopendekezwa wakati wa mkutano wa Umoja wa Wabunge Wanawake
uliofanyika mjini Dodoma leo 3 Septemba, 2014.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Sophia Simba
akichangia mada wakati wa mkutano wa Umoja wa Wabunge Wanawake kuhusu maandiko
ya kisera na manufaa waliyopata wanawake katika Rasimu ya mwisho ya Katiba
inayopendekezwa uliofanyika mjini Dodoma leo 3 Septemba, 2014.
Waziri wa Katiba na Sheria ambaye pia ni mjumbe wa
Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Asha-Rose Migiro akichangia mada leo mjini Dodoma
kuhusu maandiko ya kisera na manufaa waliyopata wanawake katika Rasimu ya
mwisho ya Katiba inayopendekezwa uliofanyika mjini Dodoma leo 3 Septemba, 2014.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Felister Bura
akichangia mada wakati wa mkutano wa Umoja wa Wabunge Wanawake kuhusu maandiko
ya kisera na manufaa waliyopata wanawake katika Rasimu ya mwisho ya Katiba
inayopendekezwa uliofanyika mjini Dodoma leo 3 Septemba, 2014.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Dkt. Angelina
Samike akichangia mada wakati wa mkutano wa Umoja wa Wabunge Wanawake kuhusu
maandiko ya kisera na manufaa waliyopata wanawake katika Rasimu ya mwisho ya
Katiba inayopendekezwa uliofanyika mjini Dodoma leo 3 Septemba, 2014.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Zainab Gama
akichangia mada wakati wa mkutano wa Umoja wa Wabunge Wanawake kuhusu maandiko
ya kisera na manufaa waliyopata wanawake katika Rasimu ya mwisho ya Katiba
inayopendekezwa uliofanyika mjini Dodoma leo 3 Septemba, 2014.
Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba
wakifuatilia mada na michango mbalimbali iliyokuwa ikiwasilishwa na baadhi ya
wajumbe wa bunge hilo leo mjini Dodoma kuhusu maandiko ya kisera na manufaa
waliyopata wanawake katika Rasimu ya mwisho ya Katiba inayopendekezwa
uliofanyika mjini Dodoma leo 3 Septemba, 2014.
Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakifuatilia mada na michango mbalimbali iliyokuwa ikiwasilishwa na baadhi ya wajumbe wa bunge hilo leo mjini Dodoma kuhusu maandiko ya kisera na manufaa waliyopata wanawake katika Rasimu ya mwisho ya Katiba inayopendekezwa uliofanyika mjini Dodoma leo 3 Septemba, 2014.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ambaye
pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Fenella Mukangara (kulia)
akisalimiana na mjumbe mwenzie wa Bunge hilo, Mhe. Angellah Kairuki mara baada
ya kumalizika kwa mkutano wa Umoja wa Wabunge Wanawake kuhusu maandiko ya
kisera na manufaa waliyopata wanawake katika Rasimu ya mwisho ya Katiba inayopendekezwa
uliofanyika mjini Dodoma leo 3 Septemba, 2014.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Dkt. Mary
Mwanjelwa (kulia) akibadilishana mawazo na mjumbe mwenzie wa bunge hilo, Mhe.
Martha Mlata mara baada ya kumalizika kwa mkutano kuhusu maandiko ya kisera na
manufaa waliyopata wanawake katika Rasimu ya mwisho ya Katiba inayopendekezwa
wakati wa mkutano wa Umoja wa Wabunge Wanawake uliofanyika mjini Dodoma leo 3
Septemba, 2014.
Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba
wakimshangilia Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta mara
walipokutana nae nje mara baada ya kumaliza mkutano wao kuhusu maandiko ya
kisera na manufaa waliyopata wanawake katika Rasimu ya mwisho ya Katiba
inayopendekezwa uliofanyika mjini Dodoma leo 3 Septemba, 2014. (Picha zote
na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma)
03/09/2014.
UMOJA wa Wabunge Wanawake Tanzania (TWPG)
wamejipongeza kwa hatua kubwa waliyofikia na manufaa waliyoyapata wanawake
katika Rasimu ya mwisho ya Katiba inayopendekezwa.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Wabunge hao
ambao pia ni Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakati walipofanya semina
iliyoandaliwa kwa ajili ya wajumbe hao kuhusu maandiko ya kisheria na manufaa
waliyopata wanawake katika Rasimu ya mwisho ya Katiba inayopendekezwa.
Akitoa mada wakati wa Semina hiyo, Katibu Mkuu wa TWPG
ambaye pia ni Mjumbe wa bunge hilo, Mhe. Angellah Kairuki amesema kuwa moja ya
manufaa ambayo wanawake watayapata katika Katiba mpya ijayo ni kuhusu masuala
ya uongozi ulio bora wenye kuzingatia sifa na weledi katika michakato ya ajira
na uteuzi ambapo suala hilo limetiliwa nguvu katika Ibara ya 208, Ibara ndogo
ya kwanza kipengele C ambapo katika masuala ya uteuzi na mambo ya ajira katika
nafasi mbalimbali katika Utumishi wa Umma utazingatia uwezo wa kitaaluma,
weledi, ujuzi, usawa wa jinsia hivyo suala la usawa wa jinsia limezingatiwa.
Mhe. Kairuki ameongeza kuwa, katika Sura ya Kumi
inayohusu masuala ya Bunge kama ilivyoelezwa katika Ibara ya 129 ibara ndogo ya
Nne, amesema kuwa kwa kutambua kuwa Bunge ndiyo mhimili muhimu wa dola, Katiba
inayopendekezwa imekusudia kurekebisha kasoro iliyopo ya uwakilishi mdogo wa
wanawake bungeni ambapo hivi sasa kuna asilimia 36.6% ya wanawake bungeni.
“Kupitia Katiba hii inayopendekezwa kupitia Ibara ya
129 Ibara ndogo ya Nne tutakuwa na uwakilishi uliosawa baina ya Wabunge
wanawake na Wabunge wanaume”, alisema Mhe. Kairuki.
Aidha, alieleza kuwa katika Sura ya 12 inayohusu
Mahakama ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tume ya Utumishi wa Mahakama
imepewa wajibu katika ajira mbalimbali na uteuzi kuhakikisha kuwa inazingatia
usawa wa jinsia.
Naye Mhadhiri Msaidizi wa Sheria kutoka Chuo Kikuu cha
Iringa, Bw. Dunford Mpelumbe amewapongeza wajumbe hao wanawake kwa kazi kubwa
walioifanya katika kudai haki zao huku akizungumzia juu ya baadhi ya Mikataba
ambayo Tanzania imeridhia pamoja na baadhi ya itifaki za Kimataifa yakiwemo
maazimio mbalimbali ambayo Tanzania kama Mwanachama wa Jumuiya ya Kimataifa
imeridhia na hatua kubwa iliyopiga.
Mpelumbe amesema kuwa katika Azimio la 1948 (Universal Declaration of Human Rights) katika
Ibara yake ya kwanza inaelezea juu ya mambo ya usawa kati ya mwanamke na
mwanaume, lakini pia suala la usawa kati ya binadamu wote umepewa kipaumbele.
Mpelumbe ameongeza kuwa licha ya Mikataba ya Kimataifa
pamoja na sheria mama zilizopo sasa nchini, haki za wanawake zinatakiwa
kujengewa ulingo wa kuzisemea mara kwa mara ili watu wapate kuzielewa vizuri.
“Nchi za wenzetu wameweka jitihada za dhati kabisa
katika kujenga uwezo wa mwanamke na jitihada hizi zinatokana na utiaji sahihi
na kuridhia hii Mikataba ya Kimataifa mbalimbali ambayo inatoa haki za wanawake
lakini hatua ya pili ni kwa kuchukua hatua za msingi za kikatiba na kisheria
kuziweka hizo haki za mwanamke katika ulingo wa Kimataifa zionekane zaidi na
kwa uwazi kabisa katika Katiba ya nchi na Sheria za nchi”, alisema Mpelumbe.
Naye Waziri wa Katiba na Sheria ambaye pia ni mjumbe
wa Bunge hilo, Mhe. Dkt. Asha-Rose Migiro amesema kuwa mshikamano ambao Wabunge
wanawake wa Bunge hilo wameuonyesha ni mkubwa sana kwani wameweza kushikamana
bila ya kujali Vyama walivyotoka, Kundi waliloliwakilisha , Sura na hata afya
zao.
Dkt. Migiro ameeleza kuwa suala la hamsini kwa hamsini
limekaa vema katika Rasimu ya mwisho ya Katiba inayopendekezwa na itawapa
wanawake wengi msingi wa kuteremka chini kwani wanawake wengi wamejitokeza kwa
wingi katika Mabaraza ya Kata na Taasisi zenye mrengo unaofanana na wamekuwa waaminifu
ndani ya Bunge Maalum.
“Katiba hii ni yenu, tutakwenda kuipigia debe kwani ni
Katiba ambayo imetuweka mahali pazuri kuimarisha haki ndani ya nchi yetu,
maslahi ndani ya taifa letu, kuimarisha Muungano wetu na umoja wetu”, alisema
Dkt. Migiro.
No comments:
Post a Comment