TANGAZO


Friday, October 24, 2014

Tottenham yatisha kombe la Uropa

Everton
Katika michuano ya Uropa mechi 12 zimechezwa usiku wa kuamkia Ijumaa ambapo Tottenham Hotspurs ya England wamewabamiza bila huruma Asteras Tripolis ya Ugiriki kwa magoli 5 -1.
Ilikuwa ni hat-trick ya Harry Kane ambayo imeisaidia Tottenham kuwabugiza magoli Wagiriki hao.
Katika upande mwingine Everton imewatunishia misuli Wafaransa, Mpaka dakika ya 90, si Lille wala Everton aliyechezea nyavu za mwenzie.
Mchezo huo uliotanguliwa na mapambano kati ya Polisi na mashabiki wa Everton ukaisha kwa sare ya bila kufungana.
Katika mechi hiyo mchezaji Chipukizi mwenye asili ya Kenya raia wa Ubelgiji, Divock Origi ameonyesha mchezo mzuri.
Matokeo mengine ni Villarreal imemchapa FC Zürich mabao 4-1.

No comments:

Post a Comment