Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Watu Wasiojiweza Tanzania (CAHPT), Mhina Shengena, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana kuhusu kuwataka watu wenye uwezo pamoja na Kampuni mbalimbali kuwasaidia katika kampeni yao ya ujenzi wa mabweni kwa Shule za Sekondri za Kata Tanzania Bara. Kulia ni Ofisa Habari wa Idara ya Habari, Maelezo, Beatrice Lyimo. (Picha na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Na
Beatrice Lyimo, Maelezo Dar
es Salaam
02.Oktoba,
2014
TAASISI
ya
Co-Operation For Assisting Handcapped People Tanzania imepanga kukusanya kiasi
cha Tsh. Bilioni 5 kwa ajili ya kufanikisha mpango wa taasisi hiyo ya kujenga mabweni
ya wanafunzi wa kike na Kiume katika Shule za Sekondari za Kata Nchini.
Wilaya ya Temeke inatajwa kuwa Halmashauri ya kwanza
itayoweza kunufaika na mpango huo kutokana
na ukubwa na idadi ya shule zilizopo katika eneo hilo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jana, Alhamisi (Okt
2, 2014) Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Mhina Shengena
alisema fedha hizo zitaweza kukusanywa kupitia harambee mbalimbali zitakazofanywa
na Ofisi yake ndani na nje ya nchi.
Kwa mujibu wa
Shengena alisema taasisi hiyo imepanga kukusanya kiasi cha Tsh. 2400 kwa mwezi kutoka
kwa kila Mtanzania pamoja na kupitia kwa waajiri na taasisi mbalimbali na mara baada
ya kufanikiwa kukusanya fedha hizo, ujenzi wa makazi ya wanafunzi hao unatarajiwa
kuanza mara moja.
“Wanafunzi wetu hususani wa kike wanaishi katika mazingira
hatarishi sana, wapo baadhi wamepanga katika makazi ya watu mara kwa mara tumekuwa tukisikia matukio ya wao kubakwa na kupewa mimba, hii yote
inatokana na ukosefu wa makazi ya kudumu” alisema Shengena.
Aidha Shengena aliipongeza Serikali kupitia Wizara ya
Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa pamoja na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa
msaada na ushirikiano wa karibu wanaonyesha kwao katika kufanikisha malengo ya Taasisi
hiyo.
Aliongeza kuwa Ofisi yake tayari imekwishafanya mawasiliano
na Watanzania mbalimbali waliopo nje ya Nchi ambao baadhi yao wameonyesha nia ya
dhati ya kusaidia harambee ya ujenzi huo, ikiwemo Watanzania wanaoishi nchini Uingereza.
Akifafanua zaidi Shengena alisema kwa Watanzania walioopo
nchini wanaweza kutuma michango yao katika Benki ya Posta Tanzania (TPB) katika
akaunti na. 016-002156 Tawi la Kijitonyama Jijini Dar esa Salaam na kwa wale
waliopo nje ya nchi watume michango hiyo katika benki ya CRDB kwa akaunti na.
01j2070153800.
Shengena alisema suluhu ya elimu bora kwa mtoto wa
kike na kiume Tanzania ni ujenzi wa mabweni, na hivyo aliwataka Watanzania wote
waguswe na kilio cha watoto hao ambao ni taifa la kesho.
Taasisi ya Co-Operation For Assisting
Handcapped People Tanzania, ni taasisi isiyo ya kiserikali iliyoanzishwa mwaka 1998
na inajishughulisha katika kusaidia makundi ya watu wasiojiweza ikiwemo yatima,
walemavu na watoto wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi.
No comments:
Post a Comment