Mashitaka katika kesi ya Oscar Pistorius yamechambua kazi za kujitolea za mwanariadha huyo, katika siku ya pili ya kusikilizwa kama akabiliwe na adhabu ya kifungo jela kwa kumuua mpenzi wake au la.
Msukumo mkuu wa Pistorius alitanguliza mbele kazi yake, mwendesha mashitaka amesema.
Mwanariadha huyo alipatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia Reeva Steenkamp mwezi uliopita- lakini aliondolewa mashitaka ya kuua kwa makusudi.
Jumatatu, mwendesha mashitaka alikasirishwa na wito uliotolewa kuwa Pistorius asifungwe jela na badala yake atumikie kifungo cha nyumbani na kufanyakazi za kijamii.
Mwendesha mashitaka Gerrie Nel alielezea pendekezo hilo kama adhabu isiyostahili.
Bi Reeva Steenkamp, mwenye umri wa miaka 29, mwanamitindo na mhitimu wa sheria, alipigwa risasi na Pistorius mara tatu kupitia mlango wa choo katika nyumba yake mjini Pretoria.
No comments:
Post a Comment