Baadhi ya Washiriki wa Kikao cha Kazi cha Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu Msingi kinachofanyika katika ukumbi wa Chimwaga, Chuo Kikuu cha Dodoma kuanzia tarehe 01-03 Oktoba, 2014.
Na Mwandishi wetu
OFISI ya Waziri Mkuu –
TAMISEMI kwa kushirikiana na Chuo cha
Serikali za Mitaa Hombolo wameandaa kikao cha kazi kuhusu Usimamizi na
Uendeshaji wa Elimu Msingi kwa Viongozi wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri
kinachofanyika katika ukumbi wa Chimwaga uliopo Chuo Kikuu cha Dodoma.
Kikao hicho cha siku tatu kinafanyika
kuanzia tarehe 01 hadi 03 Oktoba, 2014. Kikao hicho kinalenga katika kuainisha
mafanikio na chanagamoto katika
utekelezaji wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) katika sekta ya Elimu.
Mgeni Rasmi katika kikao
hicho anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Jakaya
Mrisho Kikwete.
Mada zitakazowasilishwa
katika kikao hicho ni pamoja na Wajibu na Majukumu ya Chuo cha Serikali za
Mitaa (LGTI), Pendekezo la kukibadili Chuo Kikuu Huria cha Taifa cha Tanzania
na mada juu Utekelezaji wa Mawasiliano Vijijini, Ujenzi wa Mikongo ya Mijini na
Watumiaji wa Mwisho pamoja na kuunganisha Shule na Taasisi za Umma katika
Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano.
Mada nyingine ni utaratibu
wa kushughulikia malalamiko ya wananchi na watumishi wa Umma, Miongozo ya
ujenzi: mafanikio na changamoto za ujenzi
wa shule pamoja na mada kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF).
Aidha, katika kikao hiki
kila mkoa utapata nafasi ya kutoa taarifa ya namna zilivyotekeleza dhana ya Matokeo Makubwa Sasa (BRN) katika
Sekta ya Elimu nchini.
Kikao hiki kimehusisha
Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya Wakurugenzi wa Halmashauri, Maafisa Elimu Mikoa na Wilaya pamoja na Watendaji kutoka Ofisi ya Waziri
Mkuu – TAMISEMI na Wizara ya elimu na
Mafunzo ya Ufundi.
No comments:
Post a Comment