TANGAZO


Thursday, October 9, 2014

Rais Kenyatta arejea kwa kishindo

Kenyatta alikwenda Hague kwa kikao maalum na mahakama ya ICC
Mamia ya watu kwa shangwe na vigelegele wamemkaribisha Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta baada ya kurejea kutoka kikao chake katika mahakama ya kimataifa ya ICC mjini the Hague.
Kenyatta alihudhuria kikao maalum katika mahakama hiyo Jumatano, na kuwa Rais wa kwanza aliye mamlakani kufika katika mahakama hiyo.
Mahakama hiyo ilimtaka afike mbele yake kutokana na malalalmsihi kutoak kwa kiongozi w amashitkaka kuwa serikali ya Kenya inaficha ushahihidi kuhusiana na kesi inayomkabili.
Rais Kenyatta akipokelewa na naibu wake William Ruto
Alikanusha madai ya uhalifu dhidi ya binadamu wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi nchini Kenya mwaka 2007 ambayo yalisababisha vifo vya watu 1,200 na kuwaacha wengine zaidi ya laki sita bila makao.
Kenyatta alipokelewa na idadi kubwa ya watu waliokuwa wanacheza densi pamoja na gwaridde la heshima.
Asubuhi na mapema, wafuasi wake walipanga foleni kwenye barabara ya kutoka uwanja wa kimataifa wa ndege mjini Nairobi.
Rais Kenyatta katika mahakama ya kimataifa ya ICC
Walipeperusha bendera na kusikika wakiimbia kwa shangwe na kumsifgu Kenyatta wakisema kuwa Rais wao hana hatia.
Rais aliwahutubia kwa mda mfupi umati huo wa watu ambao waliombwa kufika kumpokea rais na waziri wa usalama.
Mwandishi wa BBC aliyefika kushuhudia Rais huyo akiwasili nchini alisema kuwa Kenyatta ana wafasui wengi.

No comments:

Post a Comment