TANGAZO


Thursday, October 16, 2014

''Pistorius anastahili adhabu kali''

Wakili wa Oscar Pistorius anataka jaji ampe kifungo cha nje
Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius, ''anapaswa kupewa adhabu ya kutosha kwa kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp'', binamuye marehemu Reeva ameambia mahakama mjini Pretoria Afrika Kusini.
Kim Martin alisema Pistorius,mwenye umri wa miaka 27, anapaswa kuadhiwa vikali kwa makosa yake.
Pistorius alipatikana na kosa la mauaji bila kukusudia mwezi jana na heunda akakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 15 jela, lakini jaji anaweza kumpa kifungo cha nje au hata kumtoza tu faini.
Jaji, Thokozile Masipa, ameahirisha vikao vya mahakama hadi Ijumaa asubuhi.
Upande wa utetezi , unasema kuwa Pistorius anapaswa kupewa kifungo cha nyumbani na kuhudumia jamii kwa kosa lake , pendekzo ambalo kingozi wa mashitaka Garrie Nel ameelezea kushutushwa nalo.
Upande wa mashitaka unasisitiza Pistorius apewe kifungo jela akisema kitendo chake kimesababisha huzuni n a kadhia kubwa kwa familia.
Duru zinasema kwa sababu ya kucheleweshwa kwa kesi hiyo hukumu huenda ikatolewa mwezi ujao.

No comments:

Post a Comment