Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Mhandisi Mussa Natty (kushoto)
akizungumza na Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu wakati wa
ziara ya kujifunza masuala ya usimamizi wa taka zinazozalishwa katika
halmashauri hiyo.Kulia ni wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais na watendaji
wa halmashauri hiyo.
Naibu Waziri
wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu, akizungumza na watendaji wa kata za
manispaa ya Kinondoni(hawapo pichani) wakati wa ziara hiyo.Kulia ni Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Mhandisi Mussa Natty.
Badhi ya
watendaji wa kata mbalimbali za manispaa ya Kinondoni wakimsikiliza Naibu
Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu, wakati alipotembelea kujifunza
masuala ya usimamizi wa taka zinazozalishwa katika halmashauri hiyo.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu
(katikati) akiongozwa na Mwenyekiti wa soko la Tandale, Sultan Kiumbo kuingia
kwenye ofisi ya soko hilo, wakati alitembelea kujifunza changamoto za mazingira
zinazolikabili soko hilo. Mwenyekiti wa soko la Tandale, Sultan Kiumbo, akmueleza jambo Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu, wakati alipotembelea soko hilo kujifunza changamoto za mazingira.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu, akisalimiana na mama lishe katika soko la Tandale jijini Dar es Salaam, wakati alipotembelea soko hilo kujifunza changamoto za mazingira.
Naibu Waziri
wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu, akizugumza na muuza mbogamboga kujua
jinis anavyoshughulikia taka anazozalisha kwenye soko la Tandale jijini Dar es
Salaam, wakati alipotembelea soko hilo kujifunza changamoto za mazingira.
Mwenyekiti
wa soko la Tandale, Sultan Kiumbo, akimuonesha Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu
wa Rais, Ummy Mwalimu, mabaki ya matunda yalitupwa, wakati alipotembelea soko
hilo kujifunza changamoto za mazingira. (Picha
zote na Hussein Makame-MAELEZO)
No comments:
Post a Comment