Watu katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu wameanza kutumia mtambo wa kwanza kuwahi kutumika wa kutoa pesa mjini humo.
Mtambo huo wa benki ya Salaam Somali Bank, umewekwa katika hoteli moja na tayari umeanza kutumika na kuwaruhusu wateja kutoa dola za kimarekani.
Mtambo wenyewe uko karibu na hoteli ya kifahari ya Jazeera ambayo ina ulinzi mkali sana.
Watu wengi wameshangazwa na mashine hiyo kwa kuwa hawajawahi kuiona na hata kuitumia.
Sekta ya benki nchini Somalia, bado sio thabiti huku wafanyabiashara wengi na familia zao wakitumia vijisanduku vya siri kuweka akiba zao.
Banki hiyo imesema inajiandaa kuweka mitambo mingine ya pesa mjini humo.
Wadadisi wanasema hii ni ishara kwamba mji wa Mashambulizi ya mara kwa m ara yaliyokuwa yakifanyika mjini Mogadishu yamepungua huku angalau hali ya utulivu ikianza kushuhudiwa.
No comments:
Post a Comment