Dereva Boda boda ambao ni wananchama wa Chama cha Wananchi CUF wakiongoza msafara wa mapokezi ya Prof Ibrahim Lipumba mara tu alipo wasili Wilayani Tunduru akitokea Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.Lipumba yupo Mikoa ya Kusini inayojumuisha Ruvuma, Lindi na Mtwara kwa ziara ya siku 16
ikiwa na dhumuni la kuimarisha chama pamoja na kuhamasisha
wananchi kujitokeza katika daftari la wapiga kura na
vitambulisho vya Taifa.
Huu ni umati wa watu waliojipanga barabarani kumpokea Prof. Ibrahim Lipumba.
Wakazi wa Tunduru ambao ni wanachama wa Chama cha Wananchi CUF, wakiwa katika msafara waMwenyekiti wa chama hicho, Prof. Ibrahim Lipumba.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Prof Ibrahim Lipumba
mwenye shati jekundu na kofia nyekundu akiwapungia mkono
wanachama wa chama cha CUF mara tu baada ya kufika katika
Ofisi za CUF Wilaya ya Tunduru, Mkoani Ruvuma.
Polisi wakiwa katika ulinzi wa Prof Ibrahim Lipumba.
Naibu Mkurugenzi wa Oganaizesheni, Uchaguzi na Bunge wa Chama cha Wananchi (CUF), Shaweji Mketo akiwahutubia wakazi wa Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma,kutokufanya makosa
wakati wauchaguzi wa serikali za mitaa uliotangazwa kufanyika
Disemba 14 mwaka huu wahakikishe wanakipigia Chama cha
Wananchi CUF.
No comments:
Post a Comment