TANGAZO


Saturday, October 25, 2014

Kuna njama dhidi ya Misri asema Al-Sisi



Rais Al-Sisi akizungumza na maafisa wake kuhusu shambulio la Sinai

Rais wa Misri, Abdul Fattah al-Sisi, amesema nchi imenasa kwenye mapambano na wapiganaji Waislamu ili kulihami taifa.
Alisema hayo siku moja baada ya wanajeshi zaidi ya 30 kushambuliwa na kuuwawa katika ras ya Sinai.
Akihutubia taifa, huku amezungukwa na maafisa wakuu wa jeshi, Rais al-Sisi alisema watu wa nje wanapanga njama kubwa dhidi ya Misri.
Serikali imetangaza siku tatu za maombolezo baada ya mauaji makubwa kabisa kutokea jeshini kwa miongo kadha.
Hali ya hatari piya imetangazwa katika sehemu za Sinai.
Kati ya hatua zilizotangazwa ni amri ya kutotoka nje masaa fulani, na mpaka wa Misri na eneo la Gaza umefungwa.
Mashambulio yanayofanywa na wafuasi wa Al Qaeda dhidi ya jeshi katika Sinai yameongezeka tangu jeshi lilipompindua rais Muislamu, Mohamed Morsi, mwaka jana.

No comments:

Post a Comment