TANGAZO


Monday, October 27, 2014

Kodi ya internet yapingwa Hungary

Maelfu ya waandamanaji wakiwa wamenyanyua simu zao za mkononi juu mbele ya wizara ya uchumi wapinga dhidi ya sheria ya kutoza kodi matumizi ya internet nchini Hungary
Maelfu ya waandamanaji katika mji mkuu wa Hungary, Budapest wametaka kusitishwa kwa sheria iliyopendekezwa ya kutoza kodi matumizi ya internet.
Waandamanaji walishika simu zao za mkononi juu nje ya ofisi za wizara ya uchumi na kuzivunja vipande vipande kompyuta za zamani mbele ya milango ya ofisi za chama tawala cha Fidesz.
Waandamanaji wanasema sheria hiyo ni "kinyume cha demokrasia" na itawaathiri maskini. Mawaziri wameahidi kuweka kikomo katika kodi hiyo.
Rasimu ya sheria, iliyopendekezwa na serikali ya waziri mkuu Viktor Orban, itatoza senti 60 kwa kila gigabyte ya data inayosafirishwa.
Waandamanaji mjini Budapest, Hungary wakipinga kodi katika internet
Maelfu walinyanyua juu simu zao za mkononi nje ya jengo la wizara ya uchumi mjini Budapest
Waziri mkuu wa Hungary Viktor Orban anakabiliwa na tuhuma za utawala wa kiimla.
Lakini wengi wa waliokusanyika katika mji mkuu Budapest Jumapili wana wasiwasi kuhusu madhara yake.
Waandaji wa maandamano wamesema hatua hiyo "inafuatia wimbi la hatua zisizo za kidemokrasia zinazochukuliwa na Bwana Orban hali inayoifanya Hungary kujitenga sana na mwelekeo wa Ulaya".
Kwa upande wake chama tawala cha Fidesz kimesema kitawasilisha marekebisho ya rasimu ya sheria hiyo ili kuhakikisha kuwa malipo ya mwezi yanafikia kikomo cha florints 700 sarafu ya Hungary badala ya florints 150 kwa kila data ya gigabyte inayosafirishwa.
Licha ya migawanyiko ndani ya Fidesz, Bwana Orban ana wafuasi wengi nchini Hungary na chama chake kimeshinda uchaguzi wa aina tatu mwaka huu.
Lakini wapinzani wake wamelalamikia kile wanachoona kama kuongezeka kwa mtindo wa utawala wa kiimla na pia ukaribu alionao na Rais Vladmir Putin wa Urusi.

No comments:

Post a Comment