Oct 11, 2014
*Aanza asubuhi na kazi kibao
*Maelfu wafurika mkutano wake Iringa Mjini
*Makatibu watatu Chadema wahamia CCM
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi kwenye Uwanja wa Mwembetogwa, leo Oktoba 11, 2014, mwishoni mwa ziara yake ya kukagua na kuhimiza utekelezaji wa ilani ya CCM katika mkoa wa Iringa
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia kwenye mkutano huo.

Katibu wa Chadema, jimbo la Mufindi Kusini akitangaza kukihama Chadema na kujiunga na CCM katika mkutano huo wa hadhara uliofanyika leo, Mwembetogwa, Iringa mjini. Kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye aliyempandisha jukwaani kutangaza uamuzi huo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipokea kadi kutoka kwa Katibu Mwenezi wa Chadema katika Chuo Kikuu cha Sebastiab Koloa, Tanga, Mdillah Osward ya kutangaza kuhamia CCM katika mkutano huo uliofanyika viwanja vya Mwembetogwa leo.

Kada machachari na msomi wa Chadema Gerald John akitangaza kukihama chama hicho katika mkutano huo wa Mwembetogwa.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwasluti wananchi waliokuwa wakimshangilia alipowasili kwenye Viwanja vya Mwembetogwa, kuhutubia mkutano huo wa hadhara Iringa mjini.

Wananchi wakitoa ujumbe kupitia mabango kwenye mkutano huo wa Mwembetogwa mjini Iringa leo.
Vijana Chipukizi wa CCM, wakienda kwa ukakamavu kwenye mkutano huo wa hadhara wa Kinana uliofanyika viwanja vya Mwembetogwa leo.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akila chakula cha mchana kwa Mamalishe, mjini Iringa leo, kabla ya kwenda kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye Viwanja vya Mwembetogwa. Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu.
Mamalishe akimnawisha Kinana baada ya kula

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wanachama wa SACCOS ya Masoko Vicoba, mjini Iringa leo.
Kinana akiwasalimia wanachama wa Saccos hiyo alipoingia ukumbini kuzungumza nao mjini Iringa leo asubuhi.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikata utepe kabla ya kuingia kwenye mkutano wa Wana-Saccos hao mjini Iringa.

Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisalimia wazee, alipotembelea shina namba moja la Lucas Mkazizi eneo la Mkimbizi, Iringa Mjini leo asubuhi. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu akisalimia kinamama.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpatia maji Mjumbe wa Shina namba moja, Lucas Mkazizi, wakati yeye na msafara wake walipokunywa chai ya asubuhi nyumbani kwa mjumbe huo baada ya kikao cha shina hilo
Kinana akinywa chai nyumbani kwa balozi huyo, mtaa wa Mkimbizi, Iringa mjini.

Watoto wakiwa katika mapokezi hayo ya Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akilakiwa na wananchi alipowasili kwenye Ofisi ya CCM wilaya ya Iringa mjini leo asubuhi. (Picha zote kwa hisani ya Bashir Nkoromo-theNkoromo Blog)
No comments:
Post a Comment