TANGAZO


Tuesday, October 14, 2014

Kenya mboga kwa Morocco

Kocha wa Harambee Stars Bobby Williamson
Timu ya taifa ya Kenya ya kandanda Harambee Stars ilicharazwa kwa mabao 3-0 na Morocco kwenye mechi ya kirafiki iliyofanyika katika uwanja wa Stade De Marrakech mjini Marrakech Jumatatu usiku.
Wachezaji wa Kenya wakiongozwa na nahodha Victor Wanyama wa klabu ya Southampton ya ligi kuu ya England walisimama wima hadi dakika ya 75 chombo kilipoenda mrama wakameza mabao bila jibu.
Bao la kwanza lilifungwa na El Mahdi Karnass dakika ya 77 alipoachilia kombora ambalo kipa Arnold Origi hakuweza kulizuia baada walinzi kushindwa kumkaba vilivyo Karnass.
Mbark Boussoufa aliongeza la pili kutoka eneo la penalti na la tatu likapachikwa wavuni na Mouhcine Lajour.
Kocha wa Harambee Stars Bobby Williamson alilaumu walinzi wake ambao anasema walilegea dakika za mwisho ndiposa Morocco wakapata muanya wa kufunga mabao hayo matatu.

No comments:

Post a Comment