TANGAZO


Tuesday, October 14, 2014

Huduma za Posta zarejeshwa Somalia


Moja ya mitaa ya Somalia

Serikali ya Somalia imezindua huduma yake ya kwanza ya posta katika kipindi cha zaidi ya miongo miwili.
Pia imeanzisha anwani za makaazi nchini kote kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo.
Huduma za posta zilikwama wakati utawala wa Siad Barre kuanguka mwaka 1991.
Uanzishwaji upya wa huduma za posta ni ishara ya hivi karibuni kwamba hali ya kawaida inarejea nchini Somalia baada ya migogoro ya koo na dini kudumu kwa zaidi ya miongo miwili.

Mwananchi wa Somalia akitumia huduma ya ATM kwa mara ya kwanza mjini Mogadishu.

Wiki iliyopita, mashine ya kutolea fedha kwa mara ya kwanza kabisa ilifungwa katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.
Majeshi ya Umoja wa Afrika yanajaribu kurejesha hali ya utulivu nchini Somalia
Waziri wa Posta na Simu Mohamed Ibrahim amesema Wasomali kwa sasa wanaweza kupokea barua kutoka nje.
Awamu inayofuata ni kuwawezesha kutuma barua kwa marafiki na ndugu wanaoishi nje, amesema waziri Ibrahim.

Majeshi nchini Somalia

Bwana Ibrahim ameiambia BBC alifurahishwa na uanzishwaji upya wa huduma za posta.
Vijana wengi wa Kisomali hawajawahi kuona huduma za posta na "atafurahi sana" kuwafundisha huduma za posta ambazo zinachukuliwa kama "kitu cha kawaida katika sehemu nyingine duniani", amesema Bwana Ibrahim.
Wasomali wengi wanawasiliana kwa njia ya barua pepe na simu za mkononi au kutuma barua walizoandika kupitia kwa marafiki zao.
Umoja wa Afrika na majeshi ya serikali ya Somalia wanapambana na wapiganaji wa Kiislam wa kundi la al-Shabab.
Kundi hilo limefukuzwa katika maeneo mengi ya mjini ambayo yalikuwa ngome yao na kiongozi wake Ahmed Abdi Godane aliuawa katika shambulio la ndege za Marekani mwezi uliopita.
Hata hivyo, kundi hilo linafanya mashambulio ya kuvizia katika miji na linadhibiti maeneo kadha ya vijijini nchini Somalia.

No comments:

Post a Comment