Maafisa wa afya wa Marekani watafuatilia kwa karibu wafanyakazi wa afya ambao wamekuwa wakiwatibu wagonja wa Ebola, Afrika Magharibi, kwa mujibu wa sheria mpya.
Miongozo iliyorekebishwa kuhusu Ebola na kutolewa Jumatatu, inataka wafanyakazi wengi wa afya kuchunguzwa kwa siku 21 kama wana dalili za Ebola lakini hawatatakiwa kutengwa.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameshutumu hatua za kuwawekea watu karantini ya nguvu.
Mlipuko wa Ebola wa hivi karibuni Afrika Magharibi umewaambukiza zaidi ya watu 10,000 na kuua watu wapatao 5,000.
Tangazo la Marekanbi limetolwa baada ya muuguzi mmoja ambaye alilalamikia karantini aliyowekewa huko New Jersey kuruhusiwa kurudi nyumbani.
Akipinga mwongozo mpya, Gavana wa jimbo la New Jersey, Chris Christie ametetea hatua ya kumtenga Kaci Hickox mara aliporejea kutoka Sierra Leone. Amesema: "Hivi ndivyo tutakavyoendelea kufanya".
Msimamo wake unapingana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, ambaye mapema alisema wale wanaotaka kusaidia katika maeneo yaliyoathirika "wasiwekewe vikwazo ambavyo havina misingi wa kisayansi".
"wale waliopata maambukizi wanatakiwa kusaidiwa na si kuwanyanyapaa."
Watu hawasababishi maambukizi hadi pale dalili za Ebola zinapojitokeza.
Walio katika hatari kubwa ya maambukizi ni mtu yeyote ambaye amekusana na majimaji ya mwili wa mgonjwa wa Ebola.
Hata kama hawana dalili za Ebola, wanatakiwa kuepuka mikusanyiko mikubwa ya watu na usafiri unaowakusanya watu wengi pamoja, amesema Dk. Frieden, akiongeza kujipa karantini ya hiyari kunatosha.
Kaci Hickox alikuwa akifanya kazi na shirika la madaktari wa Medecins Sans Frontieres (MSF) nchini Sierra Leone kabla ya kurejea Marekani.
Ms Hickox amesema alijisikia kama mhalifu baada ya kuwekewa karantini huko Newark aliporejea kutoka Sierra Leone Ijumaa iliyopita.
Aliachiliwa Jumatatu na kusafirishwa kwenda nyumbani kwake Maine.
Idara ya afya ya jimbo la New Jersey imesema Bi Hickox hakupatikana na maambukizi ya Ebola baada ya kupimwa Jumamosi na hakuwa na dalili za Ebola kwa saa 24.
Bwana Christie ametetea hatua za jimbo lake za kuweka karantini na amesema kuwa Bi Hickox aliwasili Marekani akiwa na joto la homa - jambo ambalo muuguzi huyo analikanusha.
No comments:
Post a Comment