Afisa mmoja wa shirikisho la soka nchini Uingereza FA amesimamishwa kazi kwa mda wa miezi minne baada ya kumuambia refa mmoja wa kike kwamba anastahili kuwa jikoni badala ya uwanjani.
Naibu raisi wa shirikisho la soka katika kaunti ya Nothumberland John Cummings alitoa matamshi hayo kwa mkufunzi wa marefa Lucy May katika mkutano wa marefa mnamo mwezi machi.
May mwenye umri wa miaka 24 alimuuliza Cumminga kuhusu uwezekano wa kusimamia katika ligi ya kazkazini mashariki siku ya jumapili.Lakini Cummings alimwambia kwamba ataweza kulisimamia swala hilo.
Aliongezea''si kuingilii wewe lakini mda wote nitakao kuwa mzima,mwanamke hawezi kusimamia mecho katika ligi yangu'', Baadaye tume huru ya shirikisho la soka nchini humo iliamuru kwamba Cumminga ana hatia baada ya kukiuka sheria za shirikisho hilo kupitia kutumia lugha chafu kwa lengo la kudhalilisha jinsia nyengine.
Vilevile cummings amepigwa faini ya pauni 250 na ni sharti ahudhuri kikao cha mafunzoi kabla ya kuchukua tena wadhfa wake.
No comments:
Post a Comment