
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimia wananchi baada ya kuwasili viwanja vya Sokoni, katika Kijiji cha Mlola, kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye viwanja hivyo, akiwa katika ziara yake ya kukagua na kusimamia utekelezaji wa ilani ya CCM na pia kuzungumza na wananchi kuhusu kero mbalimbali kwa njia ya maswali na majibu, katika wilayani Lushoto, Mkoa wa Tanga, leo, Septemba 27, 2014. Wapili kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye ambaye ameambatana na Kinana kwenye ziara hiyo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Nape wakisalimia wananchi baada ya kuwasili viwanja hivyo vya sokoni, katika Kijiji cha Mlola.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipakia udongo wenye mbolea kwa ajili ya kuoteshea miche kwenye kitalu cha kuoteshea miche ya miti katika mradi wa kutunza mazingira katika Kijiji cha Kwesimu, Lushoto mkoani Tanga. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM, mkoa wa Tanga, Hanry Shekifu ambaye pia ni Mbunge wa Lushoto.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipanda mche kwenye kitalu cha kuoteshea miche ya miti katika mradi wa kutunza mazingira katika Kijiji cha Kwesimu, Lushoto, mkoani Tanga leo.
Kinana akikagua kitalu cha kuoteshea miche ya miti cha Kijiji cha Kwesimu, Lushoto.
Kitalu cha kuoteshea miche ya miti cha Kijiji cha Kwesimu, Lushoto mkoani Tanga.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitoka kukagua ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Mbweyi, Kata ya Malibwi, Lushoto akiwa katika ziara ya kukagua na kuhimza utekelezaji wa ilani ya CCM katika wilaya ya Lushoto, Mkoa wa Tanga, leo. (Picha zote na Bashir Nkoromo-theNkoromo Blog)
No comments:
Post a Comment