1.
Mwezeshaji wa Taasisi ya MAYEPS Tanzania
Lucas Marco (wa pili kulia) akimpongeza Mwenyekiti wa Taasisi ya MAYEPS
Tanzania Rose Mang’enya wakati wa uzinduzi wa kitabu kiitwacho “NITUNZE
NIKUTUNZE FAINALI UZEENI” hivi karibuni jijini Dar es salaam. Wa kwanza kushoto
ni Meneja wa Taasisi hiyo, John Masumba na Ofisa Habari wa Idara ya Habari, MAELEZO, Eleuteri Mangi (kulia).
(Picha na MAELEZO)
BeatriceLyimo- MAELEZO
10/09/2014
TAASISI isiyo ya
kiserikali ya MAYEPS Tanzania imezindua kitabu kiitwacho “NITUNZE NIKUTUNZE FAINALI
UZEENI”, chenye maudhui ya kuwasaidia watu wanaofanyakazi ya kujiajiri au
kuajiriwa kufanya maamuzi yaliyosahihi ili waweze kuishi maisha bora wakati
wakiwa kwenye ajira na baada ya kustaafu.
Akizungumza na waandishi
wa habari hivi karibuni jijini Dar es salaam, Meneja wa Taasisi hiyo John
Masumba amesema kuwa uzoefu unaonesha kuwa wafanyakazi katika jamii ya
Kitanzania hawaweki akiba kwa ajili ya kuwekeza kwa madhumuni ya kujenga uchumi.
Meneja Masumba amesisitiza
kuwa MAYEPS imetambua kwamba ikiandaa warsha moja kwa mwezi juu wafanyakazi kufanya
maamuzi yaliyo sahihi, itawafikia watu 600 kwa mwaka.
Kwa upande wake Mwenyekiti
wa Taasisi hiyo Rose Mang’enya aliwapitisha waandishi wa habari juu ya yaliyomo
kwenye kitabu hicho kwa kuendesha warsha fupi iliyowafungua macho waandishi hao
kuhusu namna ya kutunza fedha kuandaa maisha ya baadaye.
Akinukuu kauli ya mtaalamu
wa uongozi John Maxwell Mwenyekiti huyo alisema kuwa “Watu wanaofanikiwa na wasiofanikiwa
hawatofautiani sana kiuwezo bali wanatofautiana katika dhamira ya kufika kilele
au upeo wa uwezo wao”.
Mang’enya aliongeza kuwa
jukumu la kujenga maisha binafsi lipo kwa muhusika binafsi, hivyo, watumishi
wawe na msimamo sahihi utakaowawezesha kuwa na maisha bora.
Aidha, MAYEPS hutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa Umama na binafsi namna ya
kupanga matumizi.
No comments:
Post a Comment