TANGAZO


Tuesday, September 30, 2014

Waombwa kukoma kuandamana Hong. K

Kiongozi wa Hong Kong amesema kuwa Uchina haitabadilisha kanuni za uchaguzi
Kiongozi wa jiji la Hong Kong C Y Leung ametoa wito wa kusitishwa maandamano ambayo amesema yamedumaza shughuli katika jiji zima.
Amesema kuwa maandamano hayo hayawezi kubadil msimamo wa China juu ya mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi.
Raiya wa HK wakiwasha taa za simu zao usiku
Bwana Leung pia amekataa kuitikia wito wa kujiuzulu kwak ekutoka kwa vuguvugu lililopanga maandamano hayo.
Raiya wamekataa kuondoka mabarabarani wakitaka madiliko katika sera za uchaguzi
Wakati huo huo Marekani imesema inafuatilia kwa karibu kinachoendelea Hong Kong na imeutaka utawala kuchukua hatua.
Katika mkutano wa wanahabari msemaji wa Ikulu ya Marekani Josh Earnest amesema Marekani inaunga mkono matakwa ya watu wa Hong Kong.
Raia wa Hong Kong wakivurumushiwa moshi
Makumi kwa mamia ya waandamanaji wa Hong Kong wanaendelea na maandamano yao kwa siku nyingine tena baada ya kudhoofisha maeneo muhimu ya jiji hilo wakati wa mchana.
Maandamano hayo yamebandikwa jina maandamano ya miavuli.
Waandamanaji hao sasa wanamtaka Mkuu wa utawala wa Hong Kong Leung Chun-Ying ajiuzulu..
Wakati huo huo Marekani imesema inafuatilia kwa karibu kinachoendelea Hong Kong na imeutaka utawala kuchukua hatua.
Raiya wa Hong Kong akijiandaa kwa makabiliano na polisi
Katika mkutano wa wanahabari msemaji wa Ikulu ya Marekani Josh Earnest amesema Marekani inaunga mkono matakwa ya watu wa Hong Kong.
Waandamani wamebandika karatasi zenye ujumbe kwenye mabasi ya umma HK
"Duniani kote, na hii ni kweli katika Hong Kong na maeneo mengine, Marekani inaunga mkono kimataifa, uhuru, kama vile uhuru wa kukutana kwa amani na uhuru wa kujieleza.
Maelfu ya waandamanaji katika barabara za Hong kong
Marekani inautaka utawala wa Hong Kong kuchukua hatua, na kwa upande wa waandamanaji kutoa maoni yao kwa amani"

No comments:

Post a Comment