Baadhi ya walimu wa Shule ya Sekondari WAMA-Nakayama wakifuatilia kwa makini hotuba ya ufungunzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu haokatika masuala ya jinsia na stadi za maisha. Hotuba hiyo ilikuwa ikitolewa na Mkurugenzi wa Elimu wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Dkt. Mikidadi Alawi (hayupo pichani) tarehe 15.9.2014.
Mkuu wa Kitengo cha Uragibishi na Mawasiliano kutoka Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Ndugu Philomena Marijani akiwakaribisha walimu na wageni waalikwa wakati wa sherehe ya ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu wa Shule ya Sekondari WAMA-Nakayama iliyoko katika Kijiji cha Nyamisati huko Wilayani Rufiji yaliyofanyika shuleni hapo tarehe 15.9,2014.
Mkurugenzi wa Idara ya Elimu katika Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Dkt. Mikidadi Alawi akifungua rasmi mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu wa Shule ya Sekondari WAMA-Nakayama. Waliokaa kushoto kwake ni Ndugu Obeth Mwakatobe, Makamu Mkuu wa Shule akifuatiwa ni Mwezeshaji wa mafunzo hayo Ndugu Anitha Masaki kutoka Shirika la FAWE na Kulia kwa Mgeni rasmi ni Ndugu Philomena Marijani kutoka WAMA. Mafunzo hayo ya siku tano yalifunguliwa rasmi tarehe 15.9.2014 na yameandaliwa na Taasisi ya WAMA wakishirikiana na UNICEF.
Mwezeshaji wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu wa Shule ya Sekondari WAMA-Nakayama Ndugu Anitha Masaki kutoka Shirika la FAWE (Forum For African Women Educationalists-Tanzania Chapter) akitoa moja ya mada zake mara tu baada ya ufunguzi rasmi wa mafunzo hayo shuleli hapo tarehe 15.9.2014.
Picha ya pamoja ya washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu wa Shule ya Sekondari WAMA-
Nakayama mara baada ya ufunguzi rasmi wa mafunzo hayo tarehe 15.9.2014. (Picha zote na John Lukuwi)
Na Eleuteri
Mangi-MAELEZO
16/09/2014
WALEZI wameaswa kuwaelimisha,
kuwalinda, kuwaandaa na kuwajali watoto wa kike namna ya kupambana na
changamoto mbalimbali za kijinsia zinazowakumba watoto hao wakati wakiwe shuleni
na hata nyumbani wa likizo.
Kauli hiyo imetolewa na
Mwezeshaji kutoka TUSEME wa masuala ya Ufundishaji ambao ni Rafiki Kijinsia
Anita Masaki wakati wa semina ya siku tano kwa walimu na watumishi wasio
waalimu wa Shule ya Wasichana ya WAMA-Nakayama iliyopo kijiji cha Nyamisati walayani Rufiji
mkoa wa Pwani.
Anita amewataka walezi hao
kutambaua dhamana waliyopewa na wazazi wa watoto hao na taifa kwa ujumla ya kuwaandaa
vema wanafunzi hao kitaaluma na watambue umuhimu wao wenyewe na kwa taifa.
Kwa upande wake Mkurugenzi
wa Idara ya Elimu kwa mtoto wa kike wa taasisi ya WAMA Mikidadi Alawi
akimkaribisha Mwezeshaji wa semina hiyo alitoa taarifa fupi ya shule hiyo kuwa
ina idadi ya wanafunzi 400 tangu kuanzishwa kwake ambapo kwa sasa wapo
wanafunzi 363.
Alawi alisema kuwa
shule ya WAMA-Nakayama ilianzishwa kwa lengo la kuwalea watoto wa kike
wanaoishi katika mazingira magumu ambapo wanatoka mikoa yote nchini.
Naye Mlezi wa wanafunzi
shuleni hapo Sarah Ngonde amesema kuwa wamenufaika na semina hiyo kwa kuwa
imekuja wakati mwafaka kuimarisha maarifa yao ya namna ya kuwalea wanafunzi hao
ili kuwasaidia wafikie malengo yao na hatimaye kuwa raia wema nchini.
Sarah alisema kuwa
wanaamini watakapo maliza semina hiyo watakuwa wanajua zaidi namna ya kuangalia
masuala ya kijinjsia katika shuleni hapo na hata watakapokuwa na familia zao
nyumbani.
Shule ya Wasichana ya
WAMA-Nakayama inayomilikiwa na taasisi isiyo ya serikali ya WAMA inatoa elimu
ya sekondari kwa wasichana kidato cha kwanza hadi sita ilizinduliwa rasmi
Septemba 24, 2011 na Rais wa Serlikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwnyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Ali Mohamed Shein.
No comments:
Post a Comment